Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari

Diaspora wetu nao wadukue huko nje watuletee tatizo lao wakiwa nje wanasahau malengo yao kazi ni night club na masifa, kuleta magari nyumbani basi ni wachache wanaoinufaisha nchi na tech waliotoa nje, unajua mtu unaweza dukuliwa hata maneno unayotoa katika matamasha, warsha na semina zinazohusu serikali kama ukiendelea kuwaalika wa nje kuhusu mambo yetu natoa mfano kunakua na kikao cha TCRA kuhusu mbinu za kuzuia cyber crime lakini unakuta kuna wazungu na wa nje ambao kimsingi hawakustahili kuwepo, hivi juzi kongamano la Diaspora Zanzibar nimeona wazungu nao ndani wanasikiliza tunachosema nikashangaa sasa hawa nao wameingia kama nani si ndio kudukuliwa huko katika mikakati yetu? Mbona sisi hatuendi wakiwa na mikutano inayohusu mambo yao ya ndani?.Hayo ni maoni yangu tu
 
Kabla ya kuwaza udukuzi....tuwaze kwanza kwanini watu hawana uzalendo na nchi yao??? Nini kinatokea??? Unaweza wekeza kwenye ujasusi mwishoni ukapata double agents ikawa tatizo zaidi!!!
 
Na nchi yetu ambayo inahitajika kuwa ya viwanda ulikuwa ni muda mwafaka wa kuwa na wadukuzi ambao wangetusaidia kutoa mwelekeo wa namna gani nchi kama China au Russia zimefanikiwa katika viwanda.

Ila daaah tumekalia kuchunguza vikao vya ndani ya vyama vya siasa japo ni sehemu pia ya majukumu yao ila kwanini tutumie nguvu huku kuliko kwenye economic espionage!
 
Kabla ya kuwaza udukuzi....tuwaze kwanza kwanini watu hawana uzalendo na nchi yao??? Nini kinatokea??? Unaweza wekeza kwenye ujasusi mwishoni ukapata double agents ikawa tatizo zaidi!!!
Kutothaminiwa
Ulafi na tamaa
Kuahidiwa maisha mazuri
Kulazimishwa kufanya asichopenda kukifanya
 
ku code ninayo weza kumuunganisha mtu anae tumia tigo

kifurush cha kabang cha Tsh 49999 chenye Dk 1000 sec 10000 Mb 250 mitandao yote Mwez mzima

ila mi nitakuunganisha kwa sh 22000 tu
 

Mkuu, umeongea jambo la msingi sana.
 
Hivi kuna mtu anaeweza kupoteza mda wake kuidukua Tanzania kweli? labla Rwanda,

Tanzania kila kitu tunacho tumia kinatoka nje! Majasusi wa kimarekani wadukue IPP au Azam waibe tech ya kuchanganya juice? haha Tanzania hatuna kitu cha kuficha bhana
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kama wachina wanajua kudukua basi wadukue HQ ya Cocacola na waibe ile formula yakutengeneza Coca maana katika vitu vinavyoongoza kulindwa duniani ile formula inalindwa balaa.
 
nimependa sana bandiko lako mkuu
kama wana macho waone na wa-act on t
 
Ukiona nchi imejaa wageni wengi tena wanajishugurisha hata na njia za uzalishaji wa small scale ujue imeshadukuliwa sana tena si chini ya miaka 20. Kwa mfano Tanzania na Wachina; China inalichukulia bara la Afrika kama sehemu kubalance population yake, kusambaza watu wake ili kupunguza population nchini China. Wanaingia kwa gia ya investments and donoring ili milango iwe wazi kwao kwaajili ya kumigrate watu wao kujaa kwenye nchi za kimasikini. Professional chineses wanabakishwa nchini kwao kwaajili ya kuitanua nchi yao kitechnolojia na ki maendeleo kupambana na kasi ya rivals wao Western block while wenye ujuzi wa kati na wachini + watukutu/ wasio na mbele wala nyuma kama vibarua katika miradi yao kwenye uwekezaji wao katika nchi za kimasikini na zisizo makini katika swala zima la kimaendeleo.
Wachina waliojaa hapa nchini ni janga na matatizo yake tutayaona miaka ya karibuni tu.
Sisi kama Tanzania tumechelewa kupeleka vijana wengi kujifunza nje ya nchi chini ya programmes maalumu na kuwarudisha kwaajili ya kutumika katika maswala kama haya ya economic and technological intelligences kwa manufaa ya nchi yetu. Miaka 50 tangia tupate uhuru tungekuwa mbali sana kiuchumi.
Nampa pongezi marehemu Mwal. Nyerere kwa kuwapeleka wachache kujifunza ila hakuwa na mipango dhabiti ya kuhakikisha wote wanarudishwa kwaajili ya nchi yao. Kutokana na sera nzuri ila utendaji mbovu na ukaguzi usio makini wengi walibadilika na kuanza kuitumia nafasi hiyo kujineemesha wao na familia zao.
Tusishangae wala kujiuliza kwanini wenzetu Wamalaysia, Waimdonesia few countries to mention sasa wako katika hatua nzuri kimaendeleo kuliko nchi za kiafrika pamoja na kuchelewa au kupata uhuru sawa na nchi nyingi za kiafrika. Waliona umuhimu wa udakuzi na wakawekeza rasilimali watu na sasa wanafaidika katika economic and technological intelligences
Sisi tuendelee kupigana majungu na kutumbuana tu
 
Hivi wale wale waliogundua helikopta kule Njombe na yule mzee aliyegundua tractor kwa mota ya pikipiki kule usa river Arusha wako wapi??? wangewaendeleza tungejivunia ugunduzi wa aina yake, maana Rwanda sasa hivi wanatengeneza Laptops walimu walitokea hapa bongo UDSM pale kitivo cha tekinolojia alipokuwepo Prof Silas Rwakabamba
 
nimependa sana bandiko lako mkuu
kama wana macho waone na wa-act on t

Shukrani mkuu maana naona juzi kakamatwa mchina pale KIA na madini ya Tanzanite.

Ila ni mara ya kwanza kwa mtu kukamatwa KIA akijaribu kutorosha madini ingawa hatujaambiwa thamani halisi ya madini hayo.

Nina imani vijana wetu sasa wanafanya kazi yao ipasavyo maana hapa ni kazi tu.
 

ALMASI zenye uzito wa kilogramu 29.5 za thamani ya zaidi ya Sh bilioni 64, ambazo zilibakiza dakika tano tu kutoroshwa kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA) kwenda ughaibuni, zimetaifi shwa na serikali.

Ni jambo la kutia moyo kuona sasa vijana wetu wa Usalama na TRA , wengine wakiwa wapya kabisa kutoka vyuoni wakifanya kazi yao kwa umakini wa hali ya juu na matunda yake sasa twayaona.

Hii vita dhidi ya ujasusi wa kiuchumi na kiteknolojia ni ya watanzania wote.

Serikali ya awamu ya tano inahitaji msaada wa kila mtanzania kuiunga mkono katika jitihada zake za kutuletea maendeleo.

Big up sana.
 


UDUKUZI WAO UTAKAPOFIKIA KWENYE LEVEL YA KUCHIMBA MADINI NA VITO VYA THAMANI HALAFU WANASAFIRISHA NJE YA NCHI BILA SISI KUJUA, HAPO SASA NDIYO MIMI NITAWANYOOSHEA MIKONO!
 
Na hawa wachina walivyojaa hapa bongo bila shaka tunadukuliwa mpk uvunguni
Wachina watu Hatari sana kwa dunia ya sasa. Wanatembea tembea sehemu nyingi za Tanzania na kuacha vikamera vidogo katika sehemu muhimu zinazopitisha watu wengi. Serikali inatakiwa iwe seriously. Hawa watu wakifanikiwa sehemu nyingi tumekwisha kabisa
 
Ni changamoto kwa taifa letu pia serikali imeshindwa kuwekeza ktk technology zaidi na mbaya ni ajira za undugulization kuna watu ni wataalamu was tehama lkn bado thamani yao haipo wanabaki wanatumika ktk kampuni za kigeni......mfano mzuri na unao onyesha uzembe wa kutokuwa makini ni kudukuliwa kwa mfumo wa open university pia account ya Twitter ttcl
 
Hivi kuna mtu anaeweza kupoteza mda wake kuidukua Tanzania kweli? labla Rwanda,

Rwanda wanatengeneza nini? wanakudanganya tu huku mitandaoni kuwa Rwanda ni bora kuliko Tanzania. But in your mind that Tanzania is the best in every thing in East Afrika. Rwanda wanahudumiwa na tajiri moja wa Tanzania-Bakhlesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…