Ujenzi Bandar ya Uvuvi Kilwa Masoko kukamilika Feb 2025. Ukishakamilika CCM kuzoa kura zote mikoa ya kusini inayopakana na bahari ya Hindi

Ujenzi Bandar ya Uvuvi Kilwa Masoko kukamilika Feb 2025. Ukishakamilika CCM kuzoa kura zote mikoa ya kusini inayopakana na bahari ya Hindi

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Ilani ya chama cha Mapinduzi inatekelezwa.
---

1722358269801.png
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambao mpaka sasa umefikia asilimia 63 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwaka 2025.

Waziri Ulega amesema hayo leo Jumanne alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaofanyika wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

Amesema bandari hiyo ya uvuvi inayojengwa kwa fedha za ndani ni mradi wa kielelezo unaotekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mradi huu tuutazame kama mboni ya jicho letu ili uwe endelevu kwa maana ukikamilika utainua uchumi wa Kilwa, ukanda wa Kusini na Taifa kwa ujumla,” amesema.

“Nimefurahi hatua ni nzuri, tumepiga hatua zaidi ya nusu, muhimu kuhakikisha kazi inakwisha kwa wakati ili Watanzania waweze kuona thamani ya pesa zao, shukrani nyingi kwa rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuujenga mradi huu ambao ni wa kielelezo kwa taifa letu,” alifafanua.

Mwanahalisi
 
Huku kanda ya ziwa jengo la uwanja wa ndege kimataifa miaka 7 stori. Wacha tuone. kura hazihitajiki!
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambao mpaka sasa umefikia asilimia 63 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2025.

Waziri Ulega amesema hayo leo alipotembelea kukagua maendelea ya ujenzi wa mradi huo unaofanyika wilayani Kilwa, mkoani Lindi leo Julai 30, 2024.

Amesema bandari hiyo ya uvuvi inayojengwa kwa fedha za ndani ni mradi wa kielelezo unaotekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Mradi huu tuutazame kama mboni ya jicho letu ili uwe endelevu kwa maana ukikamilika utainua uchumi wa Kilwa, ukanda wa Kusini na Taifa kwa ujumla”, amesema

“Nimefurahi hatua ni nzuri, tumepiga hatua zaidi ya nusu, muhimu kuhakikisha kazi inakwisha kwa wakati ili Watanzania waweze kuona thamani ya pesa zao, shukrani nyingi kwa rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuujenga mradi huu ambao ni wa kielelezo kwa taifa letu”, alifafanua
IMG-20240730-WA0055.jpg
IMG-20240730-WA0057.jpg
IMG-20240730-WA0059.jpg
IMG-20240730-WA0061.jpg
IMG-20240730-WA0063.jpg
IMG-20240730-WA0065.jpg
IMG-20240730-WA0067.jpg
IMG-20240730-WA0069.jpg
IMG-20240730-WA0071.jpg
 
Patakuwepo na Viwanda vya kuchakata samaki na kuzisindika au ndio bandari tu

Kilwa Ilipaswa iwe na Viwanda karibu 10 -20 vya kusindika mazao ya Baharini na kuzisafirisha nje ya nchi

Yaan pawe kabisa na Uwanja mzurii wa Ndege kwaajili ya kusafirisha mazao ya Baharini ndani na nje ya nchi

bandari iwe ya kufanya biashara kitaifa na kimataifa

Itakua furaha sana sana wale samaki wa Muhoro watamu sana nikawapata huku Katavi
 
kama akili zetu ni hizi hamna maana
 

Attachments

  • EkkQq3-XgAAaO8n.jpg
    EkkQq3-XgAAaO8n.jpg
    42.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom