Ujenzi gorofa na utaratibu wa mipaka

Ujenzi gorofa na utaratibu wa mipaka

Joined
Mar 15, 2021
Posts
6
Reaction score
8
Nina shida na jirani anajenga gorofa la sakafu 6, pamoja na underground parking.

Shida kubwa ni kwamba, hajafuata mwongozo wa kuacha nafasi ya kutosha kati ya jengo lake na ukuta unaotutenganisha. Hii sheria inatokea wapi?

Ningependa kuwa na uhakiki wa reference kama kuna member anafahamu. Pia ningependa kujua kama jirani ninaweza kuuliza mwonekano wa jengo.

Ili nifahamu kama baraza zinatazamia upande wangu.
 
Ha ha ha kariakoo angegombana na majirani zake wa pande zote
Nilidhania hii forum inachukulia maanani hoja na kutoa mawazo yenye umaana na ujuzi. Kuchekana na kuleteana dharau sikutegemea humu ndani. Eneo nnalozungumzia sio kariakoo, ni residential area ambayo siku hizi imepewa ubiashara kidogo. Kama hauna jibu ya swali langu, naomba usijaze hapa. Mawakili au engineers ndo watakuwa na majibu yangu. Kwa kifupi, wasomi.
 
Nina shida na jirani anajenga gorofa la sakafu 6, pamoja na underground parking.

Shida kubwa ni kwamba, hajafuata mwongozo wa kuacha nafasi ya kutosha kati ya jengo lake na ukuta unaotutenganisha.
Hii sheria inatokea wapi?

Ningependa kuwa na uhakiki wa reference kama kuna member anafahamu. Pia ningependa kujua kama jirani ninaweza kuuliza mwonekano wa jengo.

Ili nifahamu kama baraza zinatazamia upande wangu.
umesema kuna fance sasa shida nini ..

Mimi nazani badara ya kuanzisha mgogoro nae ni vizuri ukimsapoti maana kila ghrofa linalojengwa mtaani uongeza thamani ya nyumba za mtaani ..support maendeleo mzee
 
Asante kwa wazo lako. Huyu ni mchina, haitaji sapoti na wala hajitokezi kujumuika kijamii. Ningependa kufahamu na kuelewa kisheria hapa Tanzania tuna rights gani kama jirani anajenga ovyo?
 
Nilidhania hii forum inachukulia maanani hoja na kutoa mawazo yenye umaana na ujuzi. Kuchekana na kuleteana dharau sikutegemea humu ndani. Eneo nnalozungumzia sio kariakoo, ni residential area ambayo siku hizi imepewa ubiashara kidogo. Kama hauna jibu ya swali langu, naomba usijaze hapa. Mawakili au engineers ndo watakuwa na majibu yangu. Kwa kifupi, wasomi.
Anajenga Floor Ngapi?
 
Kama ana kibali cha ujenzi na ramani ina maana amezingatia vigezo ila iwapo una concern yoyte ila unaweza kwenda halmashauri ila zingatia ujirani mwema kwani unapoenda utakuwa umenzisha ugomvi binafsi.Ushauri wangu kama hajaingia kwenye eneo lako nafikiri utakuwa unasumbuana naye bure.Hilo eneo linaloachwa huachwa iwapo hamjaweka uzio kama anaweza uzio anaweka kwenye mpaka wenu.
 
Mleta uzi ameuliza swali la msingi sana na anastahili majibu sahihi. Kisheria kuna umbali unaotakiwa uachwe na kila mwenye kiwanja kutoka kwenye uzio hadi ukuta wa nyumba. Na sababu zake zinajulikana; kwani kuna huduma zinapitaga kwenye hayo maeneo na vile vile usalama kati ya jirani na jirani. Mwizi asije akotoka ghorofa moja na kurukia ghorofa nyingine. kwa sasa naona ujenzi unakiuka hiyo sheria na sababu kubwa ni mjengaji kutaka kujenga nyumba kubwa kuliko kiwanja chenyewe na wakaguzi kuzembea au kupokea chochote!
 
Nina shida na jirani anajenga gorofa la sakafu 6, pamoja na underground parking.

Shida kubwa ni kwamba, hajafuata mwongozo wa kuacha nafasi ya kutosha kati ya jengo lake na ukuta unaotutenganisha.
Hii sheria inatokea wapi?

Ningependa kuwa na uhakiki wa reference kama kuna member anafahamu. Pia ningependa kujua kama jirani ninaweza kuuliza mwonekano wa jengo.

Ili nifahamu kama baraza zinatazamia upande wangu.
Naona wivu ushakuvamia

Anakuchungulia kwa chini.....

Wivu hua unazua vita kubwa sana!

Good luck manigga!
 
Naona wivu ushakuvamia

Anakuchungulia kwa chini.....

Wivu hua unazua vita kubwa sana!

Good luck manigga!
Shida ya hii forum ni kwamba imejaa millenials na generation z wengi mno, labda hapo baadae watu wazima wengine humu ndani wenye mwelewano wa protocols na sheria za hapa na pale watapata nafasi ya kunipa mawazo yenye maana, kwa sasa nisitegemee hii forum ni utani tu naona. Inasikitika kuwa mpaka leo hii, 2022, na visomi vyote nchini, bado haiwezekani mtu kuelewa kuwa, kila mtu ana haki yake hapa nchini. Lakini naona watu humu ndani wataendelea tu na walipo, wakifikiri maendeleo yanajiotea yenyewe mitini. Safirini muone nchi zilizoendelea muelewe kwanini zinaendelea. Sio kutulia wakati unamwagiwa mchanga machoni, kisa usionekane una wivu. Kama huna jibu sio lazma uandike katika kila hoja. Jijue limits zako ujifunze kutokuandika andika hoja zisizojibu swali. Naona watu wanamda kweli!
 
Kwa Tanzania haya mambo bado sana, na uniwezekana ipo sheria sijui kama yafuatiliwa kutokana na maeneo husika.
Nakumbuka Oysterbay kuna mtu alijenga gorofa kadhaa kwenda juu, serikali ikamleta zengwe, sijui kama alilazimishwa kubomoa.

Nje ya mada, kwa mfano nchini UK, ukitakujenga ujenzi wowote utakao aidha kuongeza goroga moja juu, au undergroound, ni unaomba kibali ambacho kinategemea kama wakitokea jirani kadhaa ana kupinga, unanyimwa kibali, na wakati wa maombi unatakiwa uweke copy ya kibali nje ya nyumba yako kwa majirani kusoma unataka kujenga nini na kama wakiridhia ndio unapewa kibali kuendelea na ujenzi....
 
Shida ya hii forum ni kwamba imejaa millenials na generation z wengi mno, labda hapo baadae watu wazima wengine humu ndani wenye mwelewano wa protocols na sheria za hapa na pale watapata nafasi ya kunipa mawazo yenye maana, kwa sasa nisitegemee hii forum ni utani tu naona. Inasikitika kuwa mpaka leo hii, 2022, na visomi vyote nchini, bado haiwezekani mtu kuelewa kuwa, kila mtu ana haki yake hapa nchini. Lakini naona watu humu ndani wataendelea tu na walipo, wakifikiri maendeleo yanajiotea yenyewe mitini. Safirini muone nchi zilizoendelea muelewe kwanini zinaendelea. Sio kutulia wakati unamwagiwa mchanga machoni, kisa usionekane una wivu. Kama huna jibu sio lazma uandike katika kila hoja. Jijue limits zako ujifunze kutokuandika andika hoja zisizojibu swali. Naona watu wanamda kweli!
Kama kajenga gorofa sita,wewe jenga saba basi!

Shida ni wivu,which you are entitled to feel
 
Nina shida na jirani anajenga gorofa la sakafu 6, pamoja na underground parking.

Shida kubwa ni kwamba, hajafuata mwongozo wa kuacha nafasi ya kutosha kati ya jengo lake na ukuta unaotutenganisha. Hii sheria inatokea wapi?

Ningependa kuwa na uhakiki wa reference kama kuna member anafahamu. Pia ningependa kujua kama jirani ninaweza kuuliza mwonekano wa jengo.

Ili nifahamu kama baraza zinatazamia upande wangu.
Anakufanyia jeuri kwa sababu ya tuhela
 
Kama ana kibali cha ujenzi na ramani ina maana amezingatia vigezo ila iwapo una concern yoyte ila unaweza kwenda halmashauri ila zingatia ujirani mwema kwani unapoenda utakuwa umenzisha ugomvi binafsi.Ushauri wangu kama hajaingia kwenye eneo lako nafikiri utakuwa unasumbuana naye bure.Hilo eneo linaloachwa huachwa iwapo hamjaweka uzio kama anaweza uzio anaweka kwenye mpaka wenu.
Kibali ni swala moja na kufuata utaratibu wa Ujenzi ni jambo tofauti
 
Back
Top Bottom