DOKEZO Ujenzi hatarishi kwa maisha na usalama wa watu Goba Kinzudi

DOKEZO Ujenzi hatarishi kwa maisha na usalama wa watu Goba Kinzudi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakuu salama!

Kwa masikitiko makubwa na baada ya kujishauri kwa muda mrefu nimeamua hili kulileta hapa jukwaani pengine hili suala laweza patiwa ufumbuzi.

Ni Hivi Kuna mtu alikuwa anamiliki fremu za maduka zipatazo Karina nane zikiwa katika umbo la L_shaped ambazo zilikuwa zimejengwa chini ya ardhi yaani si ghorofa sasa sijui aliwaza nini akaamua kutoa paa akaweka slab juu na kujenga fremu nyingine juu yake hali ya kwamba foundation haikujengwa kwa ajili ya kuhimili mzigo mkubwa namna hiyo.

Funny enough kaintroduce vicolumn viwili vitatu ambavo katumia steel bars za 12mm, navyoandika hvi sasa jengo lishaanza kupata cracks, kiujumla ujenzi wake ni hatarishi sana kiasi linaweza hata kuporomoka hata kabla ya ujenzi wenyewe kuisha.

Kilichonisukuma kuandika hapa ni kwamba nafsi imenisuta baada ya kukumbuka tukio la jengo lililoporomoka Goba na kuua watu, nilipokuwa nikipita pale najisemea kimoyomoyo kwamba siku si nyingi hili jengo litacollapse kutokana na lilivokuwa linajengwa kinyume na utaratibu na kweli hazikupita siku likaporomoka. Nilijilaumu sana kutokuchukua hatua.

Katika hili chonde chonde nawaomba wenye mamlaka katika hili Muonapo hii thread tafadhalini sana naomba mchukue hatua kunusura usalama wa watu.

Location: Ukiwa unatokea Mwenge along side Bagamoyo road fika Mbuyuni ulizia mwisho wa Lami, ukifika mwisho wa lami ulizia, Majengo njiapanda ya Kanisa la Roma hapo hapo mtajionea mjengo wenyewe, mkajionee nilichokielezea hapa.

N.B sina chuki yoyote na mwenye hilo jengo
 
Pesa kuipata ukubwani. Mwisho wake ni kuunga unga tu ujenzi utazani unapika biliani na mkoleo.
 
Back
Top Bottom