Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 165
- 181
Ujenzi holela majengo katikati ya Jiji Mwanza vibali vyatolewa kwa Tsh. Milioni 50
Jiji la Mwanza chini ya Mkurugenzi wake, Kiomoni Kibamba limezidi kuchafuka na kukithiri kwa majengo yanayojengwa kiholela kutokana vibali vya ujenzi kutolewa kinyume na utaratibu.
Jiji hilo kupitia Idara ya Mhandisi limekuwa likitoa vibali vya ujenzi kiholela kwa wananchi waliofikia makubaliano ya fedha.
Jiji hilo limeanza utaratibu usiyokuwa rasmi wa kutoa vibali vya ujenzi kwa gharama ya Tsh. Milioni 50 kwa kila kibali.
Katika kipindi cha hivi karibu jiji hilo, kupitia Idara hiyo ya uhandisi inadaiwa imekuwa ikitoa vibali kwa gharama hiyo na kusababisha majengo mengi kujengwa katikati ya jiji kiholela bila kufuata taratibu za Mipango miji.
Vibali hivyo, vinatolewa na Kaimu mkuu wa Idara ya uhandisi Nalbeth Mahenge ambaye ameanza kukaimu nafasi hiyo miezi mitatu sasa.
Kumekuwapo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu na wafanyabiashara jijini Mwanza ambao wamekuwa wakinyimwa vibali kutokana na kushindwa kutoa Tsh. Milioni 50.
Baadhi ya wafanyabiashara hao ambao wameomba vibali vya kukarabati majengo yao na kunyimwa vibali wamesema ili upatiwe kibali ni lazima ufikie makubaliano na idara ya ujenzi pamoja na vigogo wengine wa jiji hilo.
"Mimi nina miezi sita sasa nafuatilia kibali cha ujenzi na kingine cha ukarabati lakini mpaka sasa sijapewa kibali kutokana na kushindwa kukubaliana nao.
"Wai wanahitaji fedha nyingi Milioni 50 na mimi nilikuwa na pesa inayoelekezwa na sheria za kulipia kibali ambayo wao wanaona hawapati chochote ndio maana mpaka leo wameninyima kibali.
"Nilipoenda niliwaeleza nahitaji kibali cha ujenzi na ukarabati wa jengo langu na wameshindwa kunipa mpaka leo hii sijapewa na ukiangalia wale wote ambao wametoa fedha wamepewa vibali.
"Ukiangalia maeneo ambayo ujenzi unaendelea kiholela na sheria ya Mipango miji haijafuatwa ni pale Lebert kwenye jengo la Makanyaga, pale uhuru dampo( jengo la Salumu) na pale karibu kwa wapemba CF Builders," amesema mmoja wa wafanyabiashara walionyimwa kibali
Jengo lililopo karibu na CF builders ambalo ujenzi wake umekamilika linatajwa kuwa ni mali ya mke wa aliyekuwa mbunge wa Rorya Lameck Airo.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa utaratibu huo usiyokuwa rasmi unaofanywa na Idara ya uhandisi pamoja na mkuu wa Mipango miji pamoja na vigogo wengine wa jiji hilo unafanywa kwa maslahi yao binafsi.
Kutokana na tamaa hiyo ya watumishi wa Jiji la Mwanza, kunatajwa kusababisha jiji hilo kuwa na majengo mengi yanayojengwa kiholela huku viongozi wenye mamlaka ya kuzuia hali kuendelea wakishindwa kuchukua hatua.
.....................................................................