KERO Ujenzi holela wa fremu za maduka kila kona, mipango miji wanafanya kazi gani?

KERO Ujenzi holela wa fremu za maduka kila kona, mipango miji wanafanya kazi gani?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hii sio sawa fremu zinajengwa kila sehemu kila kona, hivi wanaohusika na mipango miji wapo kweli? Mji mkubwa kama Dar es Salaam hili limekuwa kiboko, hivi matumizi ya ardhi yapo kweli?

Yaani sasa hvi hakuna maeneo ya makazi na maeneo ya biashara, kila sehemu ni biashara tu mafremu yanajengwa tena bila utaratibu wowote.

Hao wanaotoa vibali vya ujenzi wapo makini kweli?
 
Majority ya watanzania ni wachuuzi na madalali sasa serikali na mipango miji ikiingilia kwenye ubangaizaji wa hawa watu wakati hawana option ya kuwapa itaingilia kwenye bahati waliyonayo ya kutokushinikizwa ili watunge sera za kutoa ajira zenye ujira...
 
Hii sio sawa fremu zinajengwa kila sehemu kila kona, hivi wanaohusika na mipango miji wapo kweli? Mji mkubwa kama Dar es Salaam hili limekuwa kiboko, hivi matumizi ya ardhi yapo kweli?

Yaani sasa hvi hakuna maeneo ya makazi na maeneo ya biashara, kila sehemu ni biashara tu mafremu yanajengwa tena bila utaratibu wowote.

Hao wanaotoa vibali vya ujenzi wapo makini kweli?
Nafuu nawewe umeliona halafu baada ya miaka mtano mpaka 10 bomoabomoa inapita zinavunjwa

Hii nchi inachelewa sana kustuka na kufanya yaliyo sahihi...mpaka unajiuliza hivi Mipango miji na jiji kazi yao ni ipi huku wanalipwa mishahara
 
Hiyo ndo bongo, ilishakosewa kitambo sana.
Kuirekebisha inahitaji nguvu ya ziada.

Kumbuka kuna wapinzani, ukisema suu hata kwa wema watatafuta namna wakupinge, kuna chawa hawa hata ukifanya vibaya utaambiwa unaupiga mwingi, bila kusahau kuna wafia fursa hawa penye udhia hupenyeza rupia jambo lolote kwao ni fursa kwa namna fulani...
 
Mleta mada anasahau Kwamba Karikaoo ilipangwa na Mkoloni kuwa Makazi ya Watu weusi na Viwanja havikuzidi sq.m 300.

Kwa sasa Karikaoo yote ni Commercial hub.Sinza vilikuwa Viwanja vya Makazi,sasa vinageuka kuwa commercial.

Kama Kiwanja Matumizi yake ni Makazi na biashara sioni shida Mtu Kujenga frame. Kama ni Makazi utaratibu ni Kuomba kubadili Matumizi.
 
Unakuta mtu kajaza mafremu mtaani uchochoroni kabisa, mpaka unajiuliza huyu mtu anawaza nini? Mbongo akiona tu barabara anawaza fremu, mbaya zaidi hata soko lake kwa sasa ni changamoto, fremu nyingi sana mtaani ziko wazi.

Mtu kama huyo angejenga nyumba/vyumba vya kupangisha wala asingekosa wapangaji, kinachotokea ni kukosa AKILI na Exposure!
 
Hii sio sawa fremu zinajengwa kila sehemu kila kona, hivi wanaohusika na mipango miji wapo kweli? Mji mkubwa kama Dar es Salaam hili limekuwa kiboko, hivi matumizi ya ardhi yapo kweli?

Yaani sasa hvi hakuna maeneo ya makazi na maeneo ya biashara, kila sehemu ni biashara tu mafremu yanajengwa tena bila utaratibu wowote.

Hao wanaotoa vibali vya ujenzi wapo makini kweli?
Kwa dar watu wapo kimaokoto zaidi yani zitaendelea kujengwa kila kona
 
Ukiamua chumba chako unavunja dirisha unaweka mlango unafungua duka. Mipango miji wenyewe wanasubiri kupangiwa
 
Wanajenga haijaisha wanalala humo na kupangisha, mtaa ukichangamka zinageuka Frem, mambo yakiyumba wanafugia kuku, utitiri ukija wanayageuza madarasa ya Nursery na Tuition.
 
Back
Top Bottom