Ujenzi huu utanigharimu Tshs ngapi?

Habari

Nataka kujenga chumba (master) na sebule pamoja na choo cha nje itanigharimu Tshs ngapi mpaka kufika kwenye renta ?

Karibuni wenye uzoefu
Lipia tofali
Lipia cement lipia nondo
Shusha mchanga
Lipia na bati kabisa alaf baki na hela ya Fundi m5 itakua imekata

Kama uko dar lakini utanunua hadi mbao
 
Habari

Nataka kujenga chumba (master) na sebule pamoja na choo cha nje itanigharimu Tshs ngapi mpaka kufika kwenye renta ?

Karibuni wenye uzoefu
Watu wengi watakutisha humu.

Mimi nina kauzoefu kidogo kakujenga hivi vijumba vidogo vidogo kwa kijumba hicho mtafute kwanza fundi mweleweshe aina ya material unayotaka kutumia gharama itaongezeka kulingana na sehemu ulipo. Ila kwa hicho kijumba hakitavuka millioni 5 kutegemea na material utakayotumia.
 
Kama tayari una kiwanja andaa milioni tano kwa kuanzia, simamia ujenzi na hakikisha vitu vingi unanunua kwenye maduka ya beo nafuu, fanya window shopping kwanza.
Choo: Kuchimba, kujengea, kufunika, kujengea chumba, mlango, nondo, cement, bati, mbao, ufundi, mchanga, misumari itagharimu 2m. Rooms mbili: tofali 1500, mchanga 300k, cementi mifuko 30,kokoto lori moja, mbao 400k, bati 30, player, skimming , rangi, choo, umeme, maji, milango 3, dirisha5, grill 5, vitasa 3, Blandering, gypsum board 8, ufundi. 10m imekatika.
 
10M chumba na sebule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…