Chum Chang
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 999
- 272
Udongo wa mfinyanzi una tabia ya kuhifadhi maji yanayoufanya ukose ule uimara wake,pia maji yanapokauka unatanuka na wakati mwingine kusababisha nyufa nyingi nyingi.Katika uzoefu wangu wa kujenga kwenye udongo wenye asili ya mfinyanzi,nimepata matatizo yakiwemo udongo kushindwa kubeba uzito wa jengo au ufa wake kuendelea mpaka kwenye jengo.
Nini cha kufanya?
Kama una uwezo unatakiwa kuuondoa wote katika eneo unalojenga na kuleta udongo wa aina nyingine.
Kama uwezo ni mdogo unatakiwa kutumia mchanga mwingi na kuuchanganya na kiasi kidogo cha mfinyanzi.Backfilling yote hakikisha inakua ni mchaga.Hakikisha unaseparate mfinyanzi na jengo kwa kutumia mchanga.
Njia ya pili ni kuhakikisha unareinforce vizuri foundation yako kwa kutumia nondo kuepuka expansion ya clay isiambukizwe kwenye jengo lako.
Nafikiri nimekusaidia.
Inategemea unataka kujenga nyumba ya aina gani bwana Chum Chang , Ghorofa ngapi ama nyumba ya kawaida (isiyokuwa na ghorofa), angalia kipi kitakuwa na gharama ndogo,
1) kuchimba msingi wa kama mita 1.5 hadi 2, na kujenga msingi ambao pembeni yake utatakiwa kuweka material nyingine ambayo si expansive, preferably moram, msingi uwe mpana kama mita 2. kwa njia hii usitumie mchanga maana mchanga utaruhusu maji yaingie ndani na hivyo kubadilisha kiasi cha unyevu kilichomo kwa udongo. hakikisha ndani udongo wote umeuchimba na kuutoa angalau sentimeta 30 au ft 1, kisha weka udongo mwingine preferably moram hasa hasa yenye changarawe
2) Njia ya pili unaweza kufanya kama alivyoshauri Andrew Kellei kwa kufanya replacement na udongo mzuri zaidi.
3) Nakushauri utafute Civil engineer aangalie site yako visually atakushauri vizuri zaidi na bure (zaidi labda mtakaa sehemu kuchoma nyama na bia mbili tatu) ikiwa ujenzi ni nyumba ya kawaida (non-load bearing), ikiwa ni ghorofa itabidi umlipe
Nashukuru kwa msada wenu...shauri nimeupata mda muafaka kwani naanza mchakato wiki ijayo..
Nimemtafuta engineer na nategema atakayo sema na haya mlinishauri yatawezesha dhamila yangu...
Karibu Mkuu anytime, mimi ni Civil Engineer ukinihitaji ni PM tu nitakusaidia kadiri ya uwezo wangu.
Inategemea unataka kujenga nyumba ya aina gani bwana Chum Chang , Ghorofa ngapi ama nyumba ya kawaida (isiyokuwa na ghorofa), angalia kipi kitakuwa na gharama ndogo,
1) kuchimba msingi wa kama mita 1.5 hadi 2, na kujenga msingi ambao pembeni yake utatakiwa kuweka material nyingine ambayo si expansive, preferably moram, msingi uwe mpana kama mita 2. kwa njia hii usitumie mchanga maana mchanga utaruhusu maji yaingie ndani na hivyo kubadilisha kiasi cha unyevu kilichomo kwa udongo. hakikisha ndani udongo wote umeuchimba na kuutoa angalau sentimeta 30 au ft 1, kisha weka udongo mwingine preferably moram hasa hasa yenye changarawe
2) Njia ya pili unaweza kufanya kama alivyoshauri Andrew Kellei kwa kufanya replacement na udongo mzuri zaidi.
3) Nakushauri utafute Civil engineer aangalie site yako visually atakushauri vizuri zaidi na bure (zaidi labda mtakaa sehemu kuchoma nyama na bia mbili tatu) ikiwa ujenzi ni nyumba ya kawaida (non-load bearing), ikiwa ni ghorofa itabidi umlipe
Ushauri wako ni mzuri sana,lakini penye red hapo juu vipi kama huyu mtaalamu hatumii hivyo vitu?
Kuna aina mbalimbali za clay. mbaya katika majenzi ni ile inaitwa 2:1 au expanding clays, hii kina chake hufikia 2m. ukijenga hapo unakuwa umeliwa. namna ya kutambua aina hii ni kwa msaada wa engineer au soil scientist. goodluck.
Yaani hii kitu acha, bro wangu ana kajumba chake maeneo ya mbezi makabe yaani hata hajafikisha mwaka tangu ahamie ,nyumba kama kibwaya cha mzaramo jinsi ilivyo rarukararuka!Ila nashukuru huu uzi maana na mimi nina kaeneo maeneo hayo hayo sijakaendeleza tutatafutana nikishamaliza kula urojo zenji.Karibu Mkuu anytime, mimi ni Civil Engineer ukinihitaji ni PM tu nitakusaidia kadiri ya uwezo wangu.
Karibu Mkuu.Yaani hii kitu acha, bro wangu ana kajumba chake maeneo ya mbezi makabe yaani hata hajafikisha mwaka tangu ahamie ,nyumba kama kibwaya cha mzaramo jinsi ilivyo rarukararuka!Ila nashukuru huu uzi maana na mimi nina kaeneo maeneo hayo hayo sijakaendeleza tutatafutana nikishamaliza kula urojo zenji.
mkuu naomba ushauri wsko nina site ambsyo uns mchanga mwingi je inafaa kwa ujenzi wa nyumba?Karibu Mkuu anytime, mimi ni Civil Engineer ukinihitaji ni PM tu nitakusaidia kadiri ya uwezo wangu.
Inafaa kabisa Mkuu ndio maana kuna majengo maeneo ya ufukweni ambapo ni mchanga mwingi.mkuu naomba ushauri wsko nina site ambsyo uns mchanga mwingi je inafaa kwa ujenzi wa nyumba?
ahsante mkuuInafaa kabisa Mkuu ndio maana kuna majengo maeneo ya ufukweni ambapo ni mchanga mwingi.
Kikubwa lazima uhakikishe unakua na msingi imara ambao kama ukipata mawe ni mazuri, ila ukikosa uhakikishe unapata kokoto nzuri za zege.
Mtafute mtaalamu akaangalie eneo iliajue kama huo mchanga unaweza kuwa easily washed away iliakushauri.
Otherwise kwenye mchanga ni kuzuri kujenga kuliko kwenye mfinyanzi
VP tofali za kuchoma na kujengea tope badala ya cement ni imara kweli.Inafaa kabisa Mkuu ndio maana kuna majengo maeneo ya ufukweni ambapo ni mchanga mwingi.
Kikubwa lazima uhakikishe unakua na msingi imara ambao kama ukipata mawe ni mazuri, ila ukikosa uhakikishe unapata kokoto nzuri za zege.
Mtafute mtaalamu akaangalie eneo iliajue kama huo mchanga unaweza kuwa easily washed away iliakushauri.
Otherwise kwenye mchanga ni kuzuri kujenga kuliko kwenye mfinyanzi
Inategemea ukubwa wa nyumba kwa maana ya kwenda juu kwa urefu na aina ya udongo.VP tofali za kuchoma na kujengea tope badala ya cement ni imara kweli.
Naona huku nilipo kijijin majumba makubwa tu yamejengwa kwa tope
Cement inatumika kwenye lipu na plasta na sakafu ya chin tu
Karibu tenaahsante mkuu