Mimi siyo mzee wa miaka hiyo, ila wazee watakuja kuthibitisha hili.
Kuna mitaa ipo katikati ya mji huku napoishi nyumba zimechoka ila zimepangika na barabara zinaonekana zikiwa zimenyooka.
Siku moja nikawa napiga stori na mzee mmoja akaniambia hiyo mitaa haikupimwa na idara ya ardhi, bali wananchi walikuwa wanajipanga wenyewe wakiongozwa na wenyeviti wa maeneo hayo. Yaani wananchi wao kwa wao wanakaa chini wanapanga barabara ipite wapi na mwenye eneo fulani alikuwa yupo tayari kutoa eneo lake barabara ipite.
Ushuhuda wa macho yangu kipindi nakua miaka ya tisini. Nakumbuka kijijini kwetu wazee wetu walikuwa wanasimamia uchongaji wa barabara za mitaa ya kijiji kwa trekta na wakati mwingine majembe ya mikono. Mtu alikuwa haruhusiwi kujenga bila kuonana na serikali ya kijiji waamuelekeze asijenge barabarani na wananchi walitii. Leo hii makazi mapya katika kijiji chetu ni ya hovyo hovyo tu, barabara hazieleweki na pia kuna mitaa nyumba zimebanana ilimradi tu mtu aishi center kwenye changanyikeni, wakati kuna maeneo ya wazi (mashamba) ndani ya kijiji hazizidi kilomita nne kutoka center ya kijiji.
Ujenzi wa maeneo yasiyopimwa kwa sasa ni wa ajabu sana. Unakuta mtaa una nyumba za mamilioni ya pesa lakini zimepangwa hovyo hovyo, mara mbele ya nyumba ya mtu, ndipo nyuma ya nyumba nyingine. Barabara hata hazieleweki, na inafikia muda barabara ya mita moja inaishia kwenye nyumba ya mtu, yaani uchochoro.
Hata ujenge nyumba ya mamilioni ya pesa, kama hakuna miundo mbinu ya barabara na mingineyo ni kazi na bure!
Hitimisho.
Tukubaliane tu, Watanzania wa sasa ni wajuaji, wabishi, tunaangalia leo na siyo kesho na tumevurugwa kuanzia viongozi mpaka wananchi, mambo yetu ni shaghalabaghala!.
Pamoja na sababu mbalimbali zinazowafanya wananchi wajenge maeneo yasiyopimwa kwa sasa, je kwa nini maeneo mengine wananchi hawajipangi wenyewe?
Kwani wananchi hawaoni umuhimu wa barabara mpaka idara ya ardhi ije iwaeleze?
Kwa nini wananchi hatuwaheshimu wenyeviti wa mitaa kila wanapotoa maelekezo ya ujenzi mfano barabara na mwelekeo wa nyumba?
Kwa nini na viongozi wa mitaa wamekuwa matapeli wanauza hadi maeneo ambayo wananchi walikubalina kuacha barabara?
Kizazi cha sasa cha Watanzania tumeishayakanyaga! Tusubiri mabadiliko automatikale mwenyezi Mungu akipenda!