Ujenzi Majengo ya Serikali: Wahandisi Wetu Mnakwama Wapi?

Ujenzi Majengo ya Serikali: Wahandisi Wetu Mnakwama Wapi?

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Huwa siwaelewi wahandisi wa serikali wanaangalia nini wanapo design na kujenga au kujengewa majengo ya serikali. Hapa nazungumzia majengo kama mahakama, hospitali, shule, kumbi za mikutano, ofisi n.k. Kila siku yanaibuka kama uyoga lakini kwa ubora wa chini.

Andiko hili linatokana na habari kwenye blog ya Millardayo ya kuvunjwa kwa dirisha la darasa, la mojawapo ya shule iliyojengwa karibuni kwa pesa za UVIKO-19 huko mkoani Morogoro.

Hivi inakuwaje unajenga darasa halafu unaweka aluminum ya kiwango cha chini kama hicho. Hatuna mbao nzuri ambazo zingeweza kutengeneza dirisha likadumu hata miaka 50? Majengo mengi ya serikali yanawekwa vidirisha kama hivyo. Siku ya kwanza tu kutumia jengo, madirisha yanaanza kusumbua kufunguka au kufyatuka. Wale walioweka huko nyuma kiwango cha chini cha bati ya kutumia kuezeka kwenye majengo ya serikali, walisahau kuweka kiwango cha ubora wa aluminum na vioo? Vinafuatwa?

Hapo hujazungumzia ujenzi hovyo ambao hauna msingi imara, bati imara, paa, upitaji hewa, kupunguza sauti n.k.

Yaani wahandisi hapa Tanzania tuko very local, tume updgrade kidogo kutoka kwenye tembe zetu kijijini - sijui ni kukosa exposure, kuogopa gharama au upigaji. Majengo yetu yote tunayafanya kama majengo ya matumizi muda mfupi.

Unawezaje jenga jengo la serikali ambalo halitoweza dumu hata miaka mitano? Hivi sisi tutakuwa tunajenga miaka nenda rudi?

Kwanini tunajenga majengo kama mahema? Wanasiasa hawahusiki kutengeneza michoro, kukadiria gharama za ujenzi na kuweka bajeti za majengo husika. Lawama zote kwa wahandisi.

Tulinganishe yale majengo waliyotuachia wakoloni na yale tunayojenga sasa.

ddddiiii-360x220.jpg

images (16).jpeg
 
Akili zao wanazijua wenywe
Unakumbuka ujenzi wa hostel za magufuli na expanssion joint?
 
Kwa DSM Jango pekee lililojengwa kwa viwango vyote vinavyohitajika ni Jango ambalo Serena Hotel ipo,lile Jango hata nikiwa basement likitokea la kutokea Nina uhakika wa kutoka nje salama, systems zake zipo wazi na zinaonekana na zinafanya kazi, majengo mengine ni ya kupiga chini na tuanze upya
 
Uoigaji mwingi, alafu wao ndiyo mstari wa mbele kukagua majengo ya wengine na kuyakosoa...
 
Back
Top Bottom