elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
UJENZI wa meli mpya ya kisasa Ziwa Victoria umefikia asilimia 35, ambao unatarajia kugharimu Sh. bilioni 86 hadi kukamilika kwake. Hayo yameelezwa juzi jijini Mwanza na Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (Mscl) Mwanza, Abel Gwanafyo, kwa niaba ya ofisa mtendaji mkuu wa huduma hizo.
“Meli hiyo ina uwezo wa tani 400 yakiwamo magari madogo 20 na makubwa matatu na kubeba abiria 1,200, ambayo itakuwa ya kisasa zaidi kuliko meli zingine katika Ziwa Victoria,” alisema Gwanafyo.
Akizungumza katika kongamano la wasaa wa marafiki wa habari mkoani Mwanza, Gwanafyo alisema ujenzi huo ulianza mwaka 2018 na unatarajia kukamilika 2021. Gwanafyo alisema meli hiyo inajengwa na Kampuni ya Ujenzi ya GAS EntecCO Ltd kwa kuungana na Kang Nam Cooperation ya Korea Kusini pamoja na SUMA JKT ya Tanzania.
Aidha, alisema itakuwa na viti vya kisasa zaidi vya kukaa mtu mmoja mmoja kama kwenye ndege, ambayo itafanya safari zake Mwanza kwenda maeneo ya Kemondo, Bukoba, Musoma pamoja na Uganda kupitia Bandari ya Portbell. Pia inaweza kukodiwa na watalii. Alisema itatumia saa chache kukimbia kutoka Bandari ya Mwanza kwenda bandari zingine kuliko meli ya zamani Mv. Victoria inayofanyiwa ukarabatiwa.