Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wajumbe wa bodi ya Tanzania Red Cross Society wakiongozwa na Rais wa Chama hicho Mh David Kihenzile wameonesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa nyumba 35 katika wilaya ya Hanang, mkoani Manyara.
Ujenzi huu ni sehemu ya juhudi za shirika hilo kutoa msaada kwa jamii baada ya tukio la kusikitisha lililotokea Desemba 3 mwaka jana, ambapo watu wengi walipoteza makazi na wapendwa wao.
Nyumba 35 zilijengwa moja kwa moja na Chama cha msalaba Mwekundu Tanzania kama mchango wao katika kusaidia wahanga wa janga hilo.
Kwa sasa, ujenzi wa nyumba hizo umekamilika kwa asilimia 98, na inatarajiwa kuwa jamii hiyo itapata makazi salama na ya kudumu hivi karibuni.
Wajumbe hao wa bodi ya Red Cross wamefanya ziara katika Kijiji cha Wareti kilichopo wilaya ya Hanang; mkoani Manyara kufanya tathmini ya maendeleo ya mradi huo na kuonyesha kuridhika na hatua zilizofikiwa.
Rais wa Red Cross Tanzania Mh Kihenzile alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na jamii ili kuimarisha hali zao za maisha na kuhakikisha wanaweza kuishi kwa amani na usalama.
“Mradi huu ni mfano wa jinsi tunavyoweza kuungana kama jamii katika nyakati za dhiki.Tunatarajia nyumba hizi zitawawezesha wahanga kurejelea maisha yao ya kawaida na kujenga matumaini mapya,” alisema Rais Mh Kihenzile.