Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Inategemea ni wapi. Kama ni Moshi Arusha Mbeya na Lushoto zinaweza kufaa kutokana na hali ya hewa kuzikubali. Tatizo ni kwamba usalama hauzikubali maana wezi wataingia kama kwao. Hivyo fikiri kabla ya kuingia mkenge.
nyumba nyingi za ulaya na marekani hujengwa kwa mtindo huu, na wakishafunika juu yake kwa makaratasi na maplastic inaonekana bomba sana kumbe ni mbao tu na hata sakafu imesakafishwa kwa mbao.
Ujenzi huu wa gharama nafuu je, unafaa tanzania kutokana na gharama kubwa za saruji, mchanga na mengineyo?
ni wazo zuri ila sio cost effective kwa sasa, mbao expensive sana pia kuna issue ya moto....
waakti wenzetu wana bima ya nyumba na zimamoto zao nzuri sie hatuna bima halafu kuna short za umeme wako, moto wa jirani, wa magari yalioacha njia etc na zima moto zetu unaita gari inakuja baada ya saa mbili na usaini cheque 5ml uhudumiwe..... mie naona njia mbadala kama alivyopendekeza mdau hapo juu tofali za kuchoma au hydrafoam....