Ujenzi unaoendelea Barabara ya Kilwa uzingatie afya za watumiaji

Ujenzi unaoendelea Barabara ya Kilwa uzingatie afya za watumiaji

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Unapoelekea Mbagala kupitia barabara ya Kilwa utaona ujenzi unavyoendelea kwa kujenga pia njia ya mwendokasi, kuna daraja la juu pale Uhasibu na kwa kweli inapendeza haswaa.

Mkandarasi anajitahidi kukimbizana na deadline ya kazi. Lakini kuna tatizo kubwa la vumbi litokanalo na kifusi kitumikacho kwenye ujenzi huo

Masaa yote kumekuwa na foleni kibwa lakini vumbi kama tupo jangwani. Watu wengi wameanza kuugua vifua na mafua ambapo inawezekana wengi wakafa kwa hofu wakidhani wameambukizwa CORONA.

Mshauri mwelekezi anapaswa kukagua kama vigezo kuhusu afya na usalama wa wanaoitumia sasa na wanaoishi pembezoni umezingatiwa.

Kuhusu foleni nawasihi wahusika wafungue njia mbadala zitakazopunguza adha za foleni kwa wanatumiaji.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke tusaidie kwenye hili
 
mkandarasi analipwa pesa ya miamala 😆 hiyo shughuli itachukua mwaka maana hapa kuna mtu ananidai pesa yake tumekubaliana nitampa mtu ampelekee 😄 alieanzisha hizi tozo atajua hajui 😄
 
Niliona lile vimbi nilipoenda kwenye maonesho ya sabasaba. Si la nchi hii. Jamaa wabahili wa kumwaga maji
Nilipita kwa pikipiki daah nimefika ubungo na vumbi as if nimetoka Mbali sana na vumbi la kutosha
 
Back
Top Bottom