Ujenzi wa Banda la kuku

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Naomba kuuliza, je, banda la kuku wa kienyeji na chotara linahitaji madirisha makubwa sana au ya kawaida tu?

Na katika madirisha hayo, yakiwa wazi halafu kipindi cha masika mvua ya upepo ikanyesha na maji kuingia ndani ya banda.

Je, kuku hawawezi kudhurika baada ya kuloana? Au inabidi kipindi cha mvua kuziba madirisha? Kwenu wataalamu
 
Kwa kuku wa kienyeji wanahitaji madirisha ya wastani tu km haya haya ya nyumba tunazoishi kwani hawatakiwa kufugwa ndani 24 hrs( indoor system). Kwao Banda ni sehemu ya kulala tu na kutagia mayai tu. Jioni wanaingia na asbh wanatoka nje. Ukiwafuga ndani moja kwa moja huwa hawataji vizuri na wanadumaa.

Kwa upande wa Saso hawa unaweza ukawafuga ndani moja kwa moja au ukawafuga ndani lakini kukawa na sehemu ya kutembea(Semi intensive). Banda la saso linahitaji kuwa na hewa ya kutosha kwani kuku hukaa ndani kwa mda mrefu. Ni vizuri madirisha yakawa sehemu ya juu kidogo ili mvua ikinyesha maji yasiingie ndani.

Pia kwa msimu wa masika ni vema kuwa plastic nailon ili kufunika madirisha maji yasiingie ndani lakini pia msimu wa baridi husaidia kuziba madirisha na kuacha sehemu ndogo ili kuwakinga kuku na baridi hasa vifaranga.

I hope you gonna find it useful.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…