A
Anonymous
Guest
Habari za wakati ndugu zangu!
Mimi ni Mkazi wa Dar es Salaam na nianze kwa kuipongeza sana Serikali kwa kuendelea na ujenzi wa miundombinu kurahisisha usafiri japo sio kwa maeneo mengi. Leo naomba kuongelea ujenzi wa barabara za BRT unaoendelea mkoani humu. Kwa kweli ni hatua nzuri kwamba hadi sasa tumeshafikia ujenzi wa kutoka Morocco hadi Tegeta na ule wa Ubungo hadi Mwenge.
Pamoja na hatua hii nzuri mimi dukuduku langu kwa kuangalia kwa macho ya kawaida naona Mkandarasi anayejenga kipande cha Ubungo - Mwenge ni kama hafanyi kazi yake kwa weledi na analipua tofauti na Mkandarasi anayetoka Mwenge kwenda Tegeta. Yawezekana ni Mkandarasi mmoja na yeye amefanya Sub ila anayehusika kwa kipande hicho hayupo serious na kazi kwa sababu zifuatazo:
1. Kwanza usafishaji wa site tu ni mbovu sana yaani ukiangalia namna alivyosafisha kipande cha Ubungo - Mwenge na kilivyosafishwa cha Mwenge - Tegeta unabaki na maswali mengi sana kama Mkandarasi anajua anachokifanya katika ujenzi huo.
Site ya Ubungo - Mwenge ilivyosafishwa
Site ya Mwenge - Tegeta unavyosafishwa
2. Hatua zake za ujenzi naona hafuati kabisa utaratibu kwa kuweka usalama kwa wafanyakazi na watumiaji wa barabara hiyo, huku wenzake wakiwa wameweka hadi mabati kuzuia hatari yoyote, yeye anajenga bila kujali chochote.
Site ya Mwenge - Tegeta kila kinapojengwa Kituo wameweka mabati kwa ajili ya Usalama tofauti na kwa site ya Ubungo - Mwenge
3. Lakini pia ukiangalia materials anayotumia mfano matofali yanaonesha ni yale yanayopukutika yasiyo na uiamara kama ya kwenye barabara ya Tegeta - Mwenge.
Tofali za Mwenge - Ubungo
Tofali za Mwenge - Tegeta
Sasa pamoja na haya ni vema Serikali kufuatilia kwa ukaribu ujenzi huu kwani madhara yake ndio yale barabara imejengwa haijamaliza hata muda wa uangalizi tayari imeanza kuharibika au ndani ya muda mfupi inaanza kuharibika. Na baada ya hapo tunaanza tena kutengeza kwa fedha za umma. Ni uharibifu wa fedha za umma, Serikali iangalie sasa na kurekebisha huku ikituhakikishia kuwa ujenzi ule unafuata kiwango.
Yangu ndio hayo tu ndugu zangu. Yawezekana nakosea, Wataalamu mtusaidie.