Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Paschal Ambrose amemshukuru Waziri Innocent Bashungwa kwa kuendelea kutoa msukumo ili kazi mbalimbali zinazoendelea za ujenzi katika daraja hilo ziweze kukamilika na kumueleza kuwa hadi kufika mwisho wa mwezi Agosti wananchi wataruhusiwa kupita juu ya daraja huku Mkandarasi akiendelea kukamilisha kazi zilizobakia na kukabidhi Daraja hilo ifikapo mwishoni mwa Disemba, 2024.
Mwonekano wa Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) Kilometa 3.2 linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita kupita Ziwa Victoria na ujenzi wa barabara unganishi ya Kilometa 1.66 ambapo utekelezaji unaendelea na upo asilimia 90.
Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa shilingi Bilioni 716.3 zikijumuisha Malipo ya Mkandarasi, Mhandisi Mshauri wa usimamizi wa mradi, Fidia na Usanifu. (Picha na Wizara ya Ujenzi).