Katika kuleta uimara wa ghorofa lako mkuu, mambo mawili ni hasa kwenye kusimamisha frame ya jengo (nguzo, beams, msingi na slabs):-
1. Matumizi sahihi ya nondo
2. Aina ya materials utakazo tumia wakati wa kuchanganya zege.
Sasa Kwa kuwa unahitaji kujua aina ya kokoto, hilo ni jambo katika issue ya material.
Kokoto ndio ingredient kubwa sana katika mchanganyiko wa zege, kokoto huchukua nafasi ya ujazo mara mbili zaidi ya nafasi ya mchanga ili kusaidia kuzuia nguvu ya mgandamizo (compressive strength) wakati Cement ikisimama kama kiunganishi tu cha mchanga na kokoto ili kuleta zege, hivyo umakini mkubwa unahitajika sana ili kuhakikisha unapata kokoto imara.
Hapa unatakiwa kupata kokoto ngumu sana ili kuhakikisha usalama na uimara wa jengo lako Kwani kokoto huzuia nguvu ya mgandamizo (compression force) hivyo nilazima ziwe ngumu Kwa sababu nguvu ya mgandamizo ni kubwa sana hasa kwenye concrete structures (majengo yenye zege kama ghorofa)
Kwa macho unaweza kujua zipi ni ngumu na zipi sio ngumu, ila kwa uhakika zaidi waweza kwenda maabara na kuzipima.
Ushauri wangu,
1. Usikubali kununua/kuchukua materials zisizo bora eti tu ni kwasababu ya bei.
2. Pata mtaalam wa kukushauri kabla ya kufanya manunuzi.
NB: kokoto za mawe ya granite ni bora sana.
Cheers 🥂
Niulize kuhusu ujenzi, i’ll Respond freely (0621003092)