Ujenzi wa kibanda siyo nyumba

Tatizo gharama za Choo zipo constant, iwe unajenga nyumba ya vyumba 4 au kimoja, mfumo wa Choo unamaliza sana hela

Lakini ukijipanga chumba kimoja kizuri kinajengeka

Pia mimi huwa siwaamini mafundi kwa asilimia zote, anaweza kukwambia hiyo hela inatosha kumbe lengo lake apate kazi, mjengo utakapoishia hapo hapo yeye hana hasara
 
Kama unalipa laki moja kodi kwa mwezi inaonesha kipato chako ni kizuri. Kwanini usijibane uongeze kidogo mkuu? gharama ya kujenga nyumba ndogo au chumba ni kubwa kuliko ya kujenga vyumba viwili au nyumba kubwa. sijui kama utaelewa
 
Fundi ujenzi huwa hakatai kazi asee
 
Nafikiri kujenga choo Cha shimo na mabanzi kwa muda kwanza huku nikijipanga taratibu
 
Kama unalipa laki moja kodi kwa mwezi inaonesha kipato chako ni kizuri. Kwanini usijibane uongeze kidogo mkuu? gharama ya kujenga nyumba ndogo au chumba ni kubwa kuliko ya kujenga vyumba viwili au nyumba kubwa. sijui kama utaelewa
Lakini yeye anasema anataka kujenga chumba kimoja tu, Huwezi jua malengo yake kwa baadae ni nini? Akiacha wazo lake la chumba kimoja na kuanza kufikiria vyumba zaidi ya kimoja tayari lengo lake la kukaa kwake hataweza kulifikia kwa Sababu 3ml ni ela nyingi lakini ni ndogo kulingana na uamuzi atakaochukua.
 
Chumba kimoja wastani kina chukua tofari 450-500 pigs hesabu tofari huko kwenu bei gani mchanga ukinunuwa canter ndogo una tosha na una baki kabisa.. Maji ya kujengea jumlisha pipa au tanki la kukodi.. Mbao za kununuwa au kukodisha kwa ajili ya kufungia mkanda wa chini na juu cement..kokoto za kiroba au canter n wewe ring binding wire misumali..mbao za 2*4 na 2*2 kwa ajili ya kupauwa chumba bati..misumari ya bati..

Hayo n baadhi ya material tu haya mtafute fundi mkubaliane nae gharama za ufundi ikiwezekana kama una nafasi msingi wa chumba chimba mwenyewe uokoe gharama mana usishangae ukaja ukaambiwa kuchimba tu msingi laki1 na ili uokowe gharama zaidi fundi usielewane kupandisha chumba kizima n kiasi gani ukifanya hivyo utalia mwambie nitakulipa kwa tofari na tofari moja kujenga Nita kulipa 350 kibarua juu yake na ufundi kwake kwa hiyo piga hesabu idadi ya tofari zidisha na hiyo hela utajuwa utamlipa bei gani
 
Fundi ameniambia tofali 650
Mchanga 2 cement 15 bati 16-18
Mawe Lori moja, maji nilipo ni bure, kibarua ni Mimi mwenyewe, Ela ya Fundi Hadi paa 200k siku tatu tunapiga Hadi lenter, madirish mawili na mlango mmoja vyote used, kibanda tayari.
 
Bado
-Mbao za kupaua
-Mbao za linta
-bati
-misumari ya kenchi na bati
-binding waya
NB:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…