Ujenzi wa kibanda siyo nyumba

unaweza kujenga ndiyo tena ukamaliza kabisa
 
Kwa nini usimpe hilo wazo hapa jukwaani kama yeye alivyofanya kwa msaada kwa wengine pia??

Isijekuwa habari za ukiweka million tatu baada ya mwezi unapata million sita.
hapana mkuu mi nataka tu nimsaidie kwenye ujenzi nione na iyo site yake kwa nia njema, kimsingi nyumba ya mil 3 inatosha kuhamia kabisa mfano chumba cha futi 10 kwa 10 kimoja kinagharimu laki 3.5 mpaka lenta kwa tofali na mchanga plus cement sasa nimeona milioni tatu inatosha vyumba viwili na sebule ila hawezi kuweka dirisha kote maana dirisha zuri la security+ aluminium ni laki 3 bati igharimu za milioni 1 + mbao.
 
Mimi namshauri ajenge foundation yenye ramani ya vyumba viwili na sebule,jiko na choo cha ndani.
Akishamaliza foundation ainue chumba kimoja kwa ajili ya kuhamia ili baadae aendelee na ujenzi pole.
Ingawa kutengeneza karo la choo litamgharimu kama mdau mmoja alivyocomment juu.
Hilo karo la choo peke yake huwa linakula zaidi ya 1.5 Milioni.
Kujenga kichumba kimoja tu eti kwa sababu ya panic ya kuwa mpangaji sio sawa.
Kama unalipa laki moja kodi kwa mwezi inaonesha kipato chako ni kizuri. Kwanini usijibane uongeze kidogo mkuu? gharama ya kujenga nyumba ndogo au chumba ni kubwa kuliko ya kujenga vyumba viwili au nyumba kubwa. sijui kama utaelewa
 
Umeona, ndiyo maana niliomba uweke hapa wazo lako. Limemsaidia mleta uzi bali hata mimi binafsi na naamini na wengine pia.
Asante sana
 
Umeona, ndiyo maana niliomba uweke hapa wazo lako. Halijamsaidia mleta uzi peke yake bali hata mimi binafsi.
Asante sana
ndiyo iliyokuwa nia yangu mkuu mimi kama nina milioni 2 tu siwezi kupanga wala kulalamika ujenzi ni mgumu maana watu wanadanganyana sana kuhusu ujenzi, niambie kwani nini nitakujibu.
 
Anaweza akaanza na cha pipa mkuu huku akivuta nguvu.

Sink ni Tsh 18,000 , Bomba Type C ni 25,000/= Tofali 8 ni 8,000/= ,Cement mfuko mmoja 13,500/= Mchanga atanunua viroba hata vitatu kwa buku na fundi akampa 20,000/= tu kumfanyia settings....Pipa anaweza kupata kati ya elfu 30 hadi 50.
 
Wewe ni fundi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…