Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Ushetu, Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani ameiomba serikali kukamilisha haraka ujenzi wa Kituo cha Polisi Ushetu ambacho kwa nguvu za wananchi kipo hatua ya msingi.
Ametoa Ombi hilo wakati akichangia hoja baada ya jibu la Naibu waziri wa mambo ya ndani Daniel Sillo leo Bungeni Dodoma juu ya ukamilishwaji wa Kituo cha Polisi Ushetu.
"Nimekuwa nikiahidiwa fedha itatengwa tangu mwaka 2021, lakini pia naibu waziri (aliyeopita) alifika katika kituo cha polisi na akaongea na Wananchi akawaahidi kwamba fedha itapatikana... kwa sababu naona kama 2025/2026 ni mbali sana....ni nini sasa mkamakti wa karibu wa serikali kukamilisha kituo hiki cha polisi?" -Cherehani
Katika Jibu la msingi la Naibu waziri wa Mambo ya ndani amesema Serikali ina mikakati thabiti ya kuunga mkono juhudi za Wananchi wa Halmashauri ya Ushetu, ambapo tayari tathmini imefanyika na kubaini kiasi kinachohitajima mpaka kituo hicho kukamilika ni TZS. Milioni 300 ambazo zitatengwa kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026.
Akijibu hoja hiyo leo Bungeni Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Mhe. Daniel Sillo amesema Serikali ina mikakati thabiti ya kuunga mkono juhudi za Wananchi wa Halmashauri ya Ushetu, ambapo tayari tathmini imefanyika na kubaini kiasi kinachohitajima mpaka kiyuo hicho kukamilika ni TZS. Milioni 300 ambazo zitatengwa kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026.