SI KWELI Ujenzi wa kiwanda kipya ya Tumbaku Morogoro unafanyika kwenye eneo la wazi kinyume cha Sheria

SI KWELI Ujenzi wa kiwanda kipya ya Tumbaku Morogoro unafanyika kwenye eneo la wazi kinyume cha Sheria

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Screenshot 2023-11-15 145650.png

Tulianza na shopping mall Dodoma, sasa tena ni kiwanda cha Tumbaku. Yasemekama wahusika ni wale wale!

Ukiingia mjini Morogoro, umbali kidogo kutoka mzunguko wa Msamvu kuelekea Iringa, unakutana na daraja la reli na pembeni yake unakuta shughuli za ujenzi wa kiwanda kipya cha Tumbaku.

Eneo hili kwa miaka mingi lilieleweka ni eneo la wazi, na kwa sheria zetu za ardhi, hakuna aliye na madaraka ya kubadili matumizi ya eneo la wazi.
 
Tunachokijua
Mkwawa Tobacco ni kiwanda kinachopatikana mkoani Morogoro ambacho hujishughulisha na biashara ya tumbaku ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Tovuti yao, matumizi ya jina la Mkwawa kwenye chapa yao yanachochewa na Kiongozi wa kabila la Wahehe, mwenye makazi yake Kalenga, mkoani Iringa, ambaye alipinga ukoloni wa Wajerumani.

Jina "Mkwawa" linatokana na Mukwava, lenyewe ni ufupisho wa jina la Mukwavinyika, likimaanisha "mshindi wa ardhi nyingi".

Madai ya kujenga kiwanda sehemu ya eneo la wazi
Novemba 6, 2023, mdau wa JamiiForums.com alichapisha uzi ambao pamoja na mambo mengine ulidai kuwa kiwanda hiki kipya kilikuwa kinajengwa kwenye eneo ambalo kwa miaka mingi linafahamika kuwa la wazi na kwa sheria zetu za ardhi, hakuna aliye na madaraka ya kubadili matumizi ya eneo la wazi.

Baada ya kuibuka kwa madai haya, JamiiForums ilifuatilia na kubaini kwamba kiwanda hiki kimekuwepo kwa muda mrefu, na sio kipya kama mtoa madai anavyobainisha.

April 28, 2023, mwanachama wa JamiiForums.com aliweka uzi unaoelezea jinsi kampuni hii ilivyoamua kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwezesha wakulima kufanya kilimo chenye tija.

Aidha, katika kufuatilia undani wake, JamiiForums ilizungumza na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Ally Machela aliyebainisha kuwa watu wanaolalamika hawajapata taarifa sahihi au wamepata taarifa za kufikirika na kwamba kiwanda hicho sio kipya, kimekuwepo kwa muda mrefu tangu enzi za mwalimu Nyerere.

"Eneo la Tumbaku kuna kiwanda kimekuwepo kwa muda mrefu tangu enzi za Mwalimu (Julius Nyerere), Kiwanda kikapitia hatua mbalimbali za umiliki kubadilika mara kadhaa, kwa sasa kinaitwa Mkwawa Tobacco Ltd" alisema Machela.

Pia, Sehemu inayozungumziwa ni eneo la kiwanda tangu enzi za Mwalimu, hakuna alipoongeza wala kupunguza, hata wakati wa chama kimoja kulikuwa na kawaida ya kuwema maeneo ya michezo mfano mpira na mingine mingi.

"Mambo yamebadilika na kiwanda hakina timu ya michezo ya mpira wa miguu wala netball, kwa kuwa eneo lipo ndani ya Kiwanda, wamiliki au mmiliki ameamua kuongeza kiwanda cha pili.

Hatua ya kuongeza kiwanda kwetu ni jambo la faraja kwa kuwa ni kiwanda cha pili kwa ukubwa kwa viwanda vya sigara upande wa Kusini mwa Jangwa la Sahara."


Hivyo, si kweli kuwa ni eneo la wazi kama inavyosemwa bali ni eneo la Kiwanda na kinachoendelea hakijavuka mipaka, fikra zilizopo ni baadhi kuwa na dhana lile ni eneo la wazi jambo ambalo si sahihi.
Back
Top Bottom