Ujenzi wa kukatakata bati na mapaa marefu unaongeza gharama za ujenzi.

Ujenzi wa kukatakata bati na mapaa marefu unaongeza gharama za ujenzi.

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Great thinkers.
Nimekuwa nikiangalia mtindo wetu wa kuezeka haya mahekalu naona kama unaongeza gharama zisizokuwa za lazima kwa mfano.

1. Nyumba yenye konakona nyingi matokeo yake mbao zinakatwakatwa vipande vingi. Bati nazo zinakatwalatwa sana. Tukumbuke viwandani wanauza bati kwa mita. Sasa vipande unavyokata na kutupa naona ni hasara.

2. Mapaa marefu.kwenda mbinguni hili nalo ni tatizo.kubwa. sawa hela ni yako sikupangii cha kufanya ila hapo unapoteza pesa nyingi kwenye materials bila sababu za msingi wengi wetu tunakimbikia mwonekano

Hivi ni baadhi ya vitu vinapelekea watu wengi waone gharama za ujenzi ni kubwa kupindukia.

IMG-20241127-WA0044.jpg

.
IMG-20241127-WA0042.jpg
465224419_3048391208647986_1484693106283140335_n.jpg
465057072_3048391051981335_9091581767378086734_n.jpg
 
Attachments

  • IMG-20241127-WA0043.jpg
    IMG-20241127-WA0043.jpg
    86.3 KB · Views: 12
Kweli,kona nyingi plus mapaa marefu zinahusisha kukatwa sana kwa mabati na kutumia bati nyingi katika ujenzi...
 
Kweli,kona nyingi plus mapaa marefu zinahusisha kukatwa sana kwa mabati na kutumia bati nyingi katika ujenzi...
Ujenzi wa siku hizi ni hasara tu maana ukibomoa nyumba huambulii chochote mabati yote ni vipande vipande.
 
Siwezi kujenga nyumba kama darasa
Kenyans wanaotuzidi mengi hushangaa sana mapaa ya Tanzania identity ya kwanza kuwa umeingia Tanzania ukitokea Ethiopia ni mabati yaliyoenda juu ungumbaru mkubwa
 
Kenyans wanaotuzidi mengi hushangaa sana mapaa ya Tanzania identity ya kwanza kuwa umeingia Tanzania ukitokea Ethiopia ni mabati yaliyoenda juu ungumbaru mkubwa
Hata wazungu hawakati katti mabati sana ni kupoteza materials. Na ni uezekaji wenye hasara kubwa
 
Back
Top Bottom