Ujenzi wa maabara aibu mkoa wa Pwani

Ujenzi wa maabara aibu mkoa wa Pwani

MPARE KIBOGOYO

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
405
Reaction score
279
Tarehe 30/6/2015 ilikuwa ndio mwisho wa kukabidhi maabara baada ya muda kubadilishwa zaidi ya mara 1, kwa visingizio kibao. Kiukweli lengo lilikuwa zuri pamoja na kupitia ujenzi huu kuna watu wamejinufaisha, upatikanaji wa fedha ulikuwa wa kimagumashi, hii imepelekea watu kufikia hata hatua ya kutoana roho kwenye halmashauri ili kupata tenda.

Pamoja na changamoto nyingi mkoa wa Pwani naamini ndio umeshika nafasi ya mwisho katika kukamilisha zoezi ili. Karibu wilaya zote hakuna hata maabara moja iliyokamilika kwa asilimia 100, Wilaya za Bagamoyo,Kisarawe na Mkuranga ndio hadi aibu..maabara nyingi zipo kwenye msingi hadi kozi ya tatu.Hivi huu mkoa nani alieuroga kielimu. Deadline imepita sisikii tamko lolote la Serikali....!
 
Back
Top Bottom