Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UJENZI WA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE KILA SEKONDARI YA KATA UNAENDELEA VIZURI
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 kwa sasa lina Sekondari 26 za Kata na 2 za Madhehebu ya Dini. Ujenzi wa Sekondari mpya 11 unaendelea kwenye baadhi ya Kata.
Ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology laboratories) unaendelea vizuri kwa Sekondari zote za Kata za Jimboni mwetu.
Ujenzi huo unachangiwa kwa ushirikiano mzuri wa Serikali, Wanavijiji na Viongozi wao.
Viongozi wa Jumuiya ya WAZAZI ya Mkoa wa Mara, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa, Ndugu Julius Kambarage Masumbo walitembelea Kata ya Nyakatende yenye sekondari mbili (Nyakatende & Kigera), na kushududia maendeleo mazuri ya miradi ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ya Kata ya Jimboni mwetu
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatano, 4.9.2024