#COVID19 Ujenzi wa madarasa kwa fedha za Uviko-19 Kuna sehemu serikali ilikosea

#COVID19 Ujenzi wa madarasa kwa fedha za Uviko-19 Kuna sehemu serikali ilikosea

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Kwa nia njema naikosoa serikali pale ambapo naona imekosea, lengo ni kujisahihisha wakati mwingine.

Hapakufanyika upembuzi mzuri wa wapi na wapi madarasa yajengwe. Ukweli mchungu ni kuwa watanzania wengi wanaishi vijijini kuliko mijini huu ukweli ambao najua viongozi wanajua.

Nimeona taarifa mbalimbali za vyombo vya habari vikiripoti Hali za shule nyingi huko vijijini zikiwa katika Hali mbaya, na hii Ni meseji kwa serikali kuwa ilipaswa nguvu nyingi za ujenzi wa madarasa mapya kufanywa huko vijijini.

Ninajua serikali haiwezi kukamilisha madarasa yote kwa pamoja, ila inaweza kuweka vipaumbele kwa sehemu ambazo Hali ni mbaya zaidi.

Shule nyingi za mijini Hali ni nzuri hivyo walipaswa nguvu kubwa kuelekeza vijijini zaidi ili kuwajengea madarasa mapya. Chini hapa nimeweka taarifa za shule ambazo hali bado ni mbaya zipo morogoro na mkoa wa kagera, wakati ujao tuanze na hawa.

Screenshot_20220125-124154_1.jpg
20220125_124145.jpg
Screenshot_20220125-124636_1.jpg
20220125_124608.jpg
 
Tozo zitakuja kutumika kujenga huko...
 
Mbuzi walifunguliwa kula, sasa wamekata kamba hata mfugaji hana muda nao
 
Back
Top Bottom