Ujenzi wa madarasa kwa hela za COVID-19 vs kupanda bei ya vifaa vya ujenzi

Ujenzi wa madarasa kwa hela za COVID-19 vs kupanda bei ya vifaa vya ujenzi

singojr

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
5,313
Reaction score
6,895
Kumetokea nini kwenye sekta ya ujenzi? Ghafla kila kitu kimepanda bei.

Je, kuna uhusiano na ujenzi wa madarasa yanayojengwa kwa kasi kipindi hiki?

Ni vifaa kuadimika kutokana na uhitaji mkubwa wa project hii?

Je, ni watu wameamua kuchezesha ili wapate kitu kwenye bei hizi mpya?

Najua serikali makini itafuatilia. Kwa hizi bei mpya ujenzi wa madarasa utakamilika kwa bajeti ile ile?

NB: Mama kuwa mkali kidogo.
 
Kuna wanafunzi wenzetu walikuwa wanasoma vyuo vya nje wamerudi kwa sababu ya covid 19 kutika nchi walizokuwa wanasoma hasa China na sasa wanajitahidi kumalizia masomo yao online/mtandaoni.

Wafadhili wao wamekata ruzuku/stipend ya kila mwezi waliyokuwa wanapewa wanafunzi hawa. Kutokana na matatizo ya umeme na masuala ya mtandao kutokuwa stable pia inawafanya kuendelea kusoma kumaliza masomo yao kuwa mgumu.

Kwa ufupi hawa ni waathirika/ wahanga halisi wa covid 19. Kwa hiyo, nashauri hela zilizotengwa ama tulizopata kwa ajili ya kusaidia waathirika wa covid vijana wetu hawa nao wepewe kipaumbele kitakachowasaidia kukabili changamoto za kumalizia shule zao.

Nadhani nimeeleweka.
 
Kwamba unabisha havijapanda?
Vimepanda ila bado bei ziko affordable japo kuna baadhi ya vitu kama gypsum powder imepanda twice..

Sababu ni kwamba uzalishaji huko Duniani ni mdogo kuliko demanda na pili freight / transport charges zimepanda Sana ..

Ukiangalia Duniani kote Chumi nyingi zime rebound post covid sasa imeleta sharp demand ndio ime push bei juu..

Yule Rais wa viwanda sijui alijenga vingapi hadi anaondoka.
 
Back
Top Bottom