Ujenzi wa madarasa salama dhidi ya radi, kufuatia vifo Bukombe ni muhimu

Ujenzi wa madarasa salama dhidi ya radi, kufuatia vifo Bukombe ni muhimu

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Geita, Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=vUhvYl7Mfww

Wanafunzi saba wa Shule ya Sekondari Businda, wilayani Bukombe wapoteza maisha huku 73 wakijeruhiwa nchini Tanzania

Tukio hilo lilitokea jana Januari 27,2025 baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha wilayani humo wakati wanafunzi wa madarasani.

Ujenzi salama unaozingatia viwango vya kukabiliana na radi vinapaswa kufanyika katika shule zote za umma na binafsi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa pole kwa Wananchi wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kufuatia ajali ya radi iliyotokea Januari 27, 2025 katika kitongoji cha Shikaliguga kata ya Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita.

Aidha, Dkt. Biteko ameelekeza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Ofisi ya Mbunge kufuatilia kwa karibu matibabu ya majeruhi wote na taratibu za mazishi ya wanafunzi hao walioaga dunia.

TOKA MAKTABA :

15 Apr 2015 — Na hiyo ndio njia traditional katika ku arrest radi. Kwa effect kubwa zaidi unachimba shimo kama mita moja chini, mita moja upana
 
Lightening Arrestor haiwezi zidi milioni moja kwa jengo moja la madarasa, sasa sijui tatizo nini haziwekwi kwenye bajeti ya ujenzi.
 
Lightening Arrestor haiwezi zidi milioni moja kwa jengo moja la madarasa, sasa sijui tatizo nini haziwekwi kwenye bajeti ya ujenzi.

Siasa nyingi kiasi, ujenzi wanafikiri ni kukamilisha kuta, paa na madarasa huku wanasahau mambo haya ya msingi na hatari kuhusu radi kwa wanafunzi wakiwa madarasani shuleni.

Inabidi majengo yote ya umma yakaguliwe kama yamewekewa mifumo inayokidhi kukabiliana na tishio la radi.
 
Uzembe wa hali ya juu Mkuu, nyumba yangu nimetumia siyo zaidi ya Sh laki nne tu, sasa sijui serikali inashindwaje ku install kwenye majengo yake hasa majengo ya shule.
 
Back
Top Bottom