SoC04 Ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu iendane na idadi ya wafanyakazi

SoC04 Ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu iendane na idadi ya wafanyakazi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Sauti haki

New Member
Joined
Oct 28, 2020
Posts
3
Reaction score
0
Miundombinu hurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii

Jamii inahitaji miundombinu bora ya barabara, maji, umeme, reli, hospitali, shule nk.

Serikali imejitahidi sana kujenga miundombinu ya kutolea elimu na afya, nipongeze sana kwa jitihada hizi. Pamoja na pongezi Kuna doa na dosari za huduma zitolewazo kutokana na uhaba wa wafanyakazi.

1. Shule nyingi mpya zimejengwa, lakini uhaba wa walimu ni mkubwa.

Hali hi inadumaza ubora wa elimu itolewayo.Wanafunzi wengi wanadahiliwa katika shule za msingi na sekondari lakini walimu wanaoajiriwa ni wachache na hawatoshelezi. Ni Vema serikali kuajiri walimu kulingana na uhitaji halisi mijini na vijijini.

2. Zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa wingi na vingine bado havijapelekewa wafanyakazi ili kuanza kutoa huduma. Kuna uhaba mkubwa wa watoa huduma ya afya katika vituo vya afya. Serikali iajiri wauguzi na madaktari kulingana na takwimu halisi za uhitaji.

Sifa haziendi kwa mtu aliyenunua gari lenye muonekano mzuri lakini haliwezi kuwaka na kutembea kwa kukosa dereva.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom