KERO Ujenzi wa NHC - Urafiki ni jambo jema, vibanda vilivyo jirani viondolewe kwani ni uchafu

KERO Ujenzi wa NHC - Urafiki ni jambo jema, vibanda vilivyo jirani viondolewe kwani ni uchafu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WASALAAM,

Napenda kumpongeza meneja wa NHC urafiki kilipokuwa kiwanda cha nguo zamani cha kanga.
anafanya kazi nzuri sana ya kurekebisha miundo mbinu na kukarabati majengo ya flats za urafiki.

Maoni ya wakazi na wafanya biashara wengi ni PLAN ya vibanda vimezagaa vikawa uchafu eneo lile, tunapendekeza viondolewe ama kutafutiwa sehemu moja yenye huduma za vyoo pia kiafya.

Pia makontena yaliyopo nyuma ya kituo cha polisi cha urafiki yamepangana mstari kwenye majengo hivyo kukosekana parking za magari, na wapangaji wa kontena hizo hawana huduma za vyoo wanajisaidia nyuma ya kontena na kuwa sehemu ya dampo za kutupia uchafu.

Pia kitendo cha kupangwa mstari plan yake haijakaa vizuri. kwa ,maoni ya wadau tungependekeza yatafutiwe eneo litengwe kwa ajili ya kuyaweka sehemu moja na kupatiwa huduma muhimu kama vyoo, n.k kama sera ya mipango miji inavyoelekeza.

Kwa kumalizia wengi wanapendekeza pia baraza ama veranda za nyumba za mbele zinazotazamana na barabara kuu ya Morogoro wengi wamesiliba wavu na mabati hivyo muonekano wa jengo kutovutia. tunashauri pia kuondolewa kwa bati na nyavu hizo ikibidi.

Swala la mabasi pia tunaomba mipangilio zaidi ya namna ya kupark na matumizi ya barabara ndogo ndogo kwani zimeharibika sana kutokana na mabasi makubwa ya abiria.

Ni imani yetu maoni yatafanyiwa kazi.

Asante
 
Back
Top Bottom