Ujenzi wa nyumba kwa kutumia tofali mbichi

Ujenzi wa nyumba kwa kutumia tofali mbichi

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Habarini wadau,

Nimetembelea mikoa ya KIGOMA, Rukwa, Katavi na kukuta wao wanapendelea tofali za kuchoma na zile za saruji! Mkoa wa Mbeya wao wanatumia hata tofali mbichi kujengea! Hivi tofali hizi ni imara kweli? Kuna utafiti wowote kuunga mkono uimara wa tofali mbichi za MBEYA?
 
Uimara unategemea Aina ya udongo ulotumka.

Ila kitaalam
Nyumba ya tope Ni imara kuliko nyumba ya saruji.
Nimeulizia hasa udongo wa Mbeya,uimara wake ukoje?Maana nilikuta watu hata fence unakuta ni tofali za tope na mvua inapiga Ila haziharibiki
 
Habarini wadau,

Nimetembelea mikoa ya KIGOMA, Rukwa, Katavi na kukuta wao wanapendelea tofali za kuchoma na zile za saruji! Mkoa wa Mbeya wao wanatumia hata tofali mbichi kujengea! Hivi tofali hizi ni imara kweli? Kuna utafiti wowote kuunga mkono uimara wa tofali mbichi za MBEYA?
Tofali mbichi???

Kiswahili kigumu sana wallah...
 
Habarini wadau,

Nimetembelea mikoa ya KIGOMA, Rukwa, Katavi na kukuta wao wanapendelea tofali za kuchoma na zile za saruji! Mkoa wa Mbeya wao wanatumia hata tofali mbichi kujengea! Hivi tofali hizi ni imara kweli? Kuna utafiti wowote kuunga mkono uimara wa tofali mbichi za MBEYA?
Kuna tafiti ilifanywa na chuo cha Mbeya Univerity of Science and Technology kikishirikiana na chuo flani cha Marekani kuangalia ubora ama uimara wa tofali za kuchoma na tofali za tope ambazo hazijachomwa kwa matumizi ya kujengea hususani kwa mkoa wa Mbeya na matokea yanaonyesha nyumba zilizojengwa na tofali mbichi ni imara ukilinganisha na tofali zikizochomwa
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla.Njoo ofisini kwetu TEGETA tukuhudumie kwa gharama nafuu sana:-
2*2 fut12=2500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=5000
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=13500
1*10fut 12 fisher board( treated)=15500
2*4 fut18(treated)=9500
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu
Mnachana na kuranda tofali pia mkuu?
 
Uimara wa nyumba ya tofali mbichi haupo. Kwanza ikinyeshewa mvua uimara wake ni sawa na kuweka mkate kwenye chai.
Kuna nyumba za makuti ziko vijijini uko Zina umri wa Miaka 200+.

Nitafutie nyumba ya saruji inayoweza dumu hata Miaka 150 tu
 
Ina maana wakoloni walipokuja hawakujua uimara wa tofali mbichi? Au huko ma NY na Paris hii elimu haipo, embu acheni mzaha
 
Ina maana wakoloni walipokuja hawakujua uimara wa tofali mbichi? Au huko ma NY na Paris hii elimu haipo, embu acheni mzaha
New York, Paris, London na miji mingi ulaya,ukiangalia majengo ya zamani ni tofali za (udongo)kuchoma...na zipo powa
 
Kuna mambo hapa watu wanachanganya

Kuna
A.Tofali mbichi (yaani tofali za tope la udongo zisizochomwa)

B.Tofali za kuchoma (yaani tofali za tope la udongo zilizochomwa)

C.Tofali za saruji (yaani za kutengeneza kwa saruji na mchanga- maarufu kama tofali za block)

Sasa mtoa mada ameuliza (kwa jinsi nilivyomuelewa) mpambano wa A na B naona watu wanahamisha mada wanapeleka mpambano kuwa B na C
 
Tofari ambazo azijachomwa ni pasua kichwa ,kilichowakuta ambao walikuwa awajaezeka ni maumivu
 
Back
Top Bottom