Ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu

Unforgettable

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2019
Posts
5,584
Reaction score
12,461
Kabla haijawekwa kwa AutoCad, toa changamoto yako hapa, nini kimekosewa, nini kipo sawa...wapi parekebishwe?

note;Fundi kanipa gharama yake ya kujenga msingi pekee kwa ukubwa huu wa nyumba ni 3M???naombeni ushauri
 
Gharama za ujenzi wa msingi zinategemea na mazingira nyumba itakapojengwa (site location). Kama eneo ni tambarare, au kuna mwinuko, au kuna bonde, au kuna miti, au visiki, au mawe, aina ya udongo na kadhalika na kadhalika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla haijawekwa kwa AutoCad, toa changamoto yako hapa, nini kimekosewa, nini kipo sawa...wapi parekebishwe?

note;Fundi kanipa gharama yake ya kujenga msingi pekee kwa ukubwa huu wa nyumba ni 3M???naombeni ushauri View attachment 2270757
Kwa nini unataka kuuweka kwenye Autocad? Nakushauri uweke mlango kati ya jiko na korido ili mtu asilazimike kupita sebuleni akitaka kwenda jikoni kutokea vyumbani na vice versa.

Amandla...
 
Kwa nini unataka kuuweka kwenye Autocad? Nakushauri uweke mlango kati ya jiko na korido ili mtu asilazimike kupita sebuleni akitaka kwenda jikoni kutokea vyumbani na vice versa.

Amandla...
shukrani
 
Hapa sitting room tv unawekaje?
Huo uwazi kati ya dinning na sitting room weka milango kama utakuwa na plan ya kuweka ac sitting room
 
naona kubwa hiyo ni gharama ya fundi tu
Mwambie akupe mchanganuo. Kufanya setting kiasi gani, kusimamia uchimbaji kiqsi gani, Zege la kwenye msingi kiasi gani, kujenga kuta za msingi kiasi gani, kujazia udongo kiasi gani, kupanga mawe, kuweka dpm na dpc kiasi gani, kunyunyizia dawa za mchwa kiasi gani, na kumwaga jamvi kiasi gani. Inabidi akueleze ufundi wake unaishia wapi ( kama hiyo gharama ni pamoja na ya vibarua au ni ya kwake yeye kama msimamizi).

Amandla...
 
Ramani yako inaonyesha hakutakuwa na mzunguko wa hewa wa kutosha.

Ndani kutakuwa kiza hakuna mwanga (vyumba vimefunga) kwa hivyo jitayarishe na mbu wengi.
 
Kwa nini unataka kuuweka kwenye Autocad? Nakushauri uweke mlango kati ya jiko na korido ili mtu asilazimike kupita sebuleni akitaka kwenda jikoni kutokea vyumbani na vice versa.

Amandla...
Hiyo pia itasaidia kuongeza mwanga kwa korido.
Nyongeze...
 
Mkuu achana na huyo fundi atakupiga. Kuna fundi mwaminifu ni mcha Mungu ametoka kunijengea nyumba yangu ningependa nikuunganishe nae kama kweli unahitaji fundi
Kabla haijawekwa kwa AutoCad, toa changamoto yako hapa, nini kimekosewa, nini kipo sawa...wapi parekebishwe?

note;Fundi kanipa gharama yake ya kujenga msingi pekee kwa ukubwa huu wa nyumba ni 3M???naombeni ushauri View attachment 2270757
 
Nadhani kama ni ufundi tu ni ghali sana, kwa namna vile tunavyojenga kibishi.
Gharama yake inalenga hadi eneo gani?
-Setting ya foundation.
-Uchimbaji wa msingi.
-Ujenzi wa msingi.
-Kusuka nondo.
-Kumwaga zege
-Kumwaga jamvi...
Lakini pia eneo lako lina topography ya aina gani?
Udongo ni wa aina gani?

Nyumba sio kubwa sana, ingekuwa mimi tungeshushana hadi 1.5m kazi yote ya msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…