Wekeni umeme kwanza. Jengeni vituo vya kisasa ndiyo muanze matangazo.Habari Njema kwa watanzania wote wapenda maendeleo.
Zoezi la Reli la utandikaji wa reli ya Standard Gauge (SGR) Sasa imeingia rasmi jijini Dar es Salaam na kwa sasa zoezi hilo linafanyika eneo la Vingunguti jijini hapa.
Naibu Waziri wa fedha amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo huku akisema mpaka sasa Serikali imeshatoa zaidi ya Trillion 2 kwenye mradi wa Reli ya SGR.
Kwa habari zaidi karibu katika youtube page ya TRC uone zaidi.
Update zitakuwa zinakuja kama kawaida mpaka ujenzi utakapo kamilikaWekeni umeme kwanza. Jengeni vituo vya kisasa ndiyo muanze matangazo.
Nakumbuka mwaka 2002 nilienda mkoa wa Kagera kwa gari ila nilienda huko kwa siku 2 tokea Dar, mara ya kwanza nililala SIngida na tukaenda lala Kahama..! Sikuhizi nasikia siku usiku mmoja tu Kahama siku ya pili unaingia Bk, Mikoa ya Lindi na Mtwara hapo nyuma walikuwa wanalala wakati ni Km 500+ lakini sikuhizi masaa 8 tu umefika Mtwara...! Sijui unawaza turudi huku ama vipi..!!Hongera Tanzania sasa nasi tunaingia kwenye maendeleo(kwa tafsiri ya sisi wanadamu).
Huwa nawaza ni kwa nini binadamu tukaamua kuwa maendeleo yahusishe kubadilisha taswira ya Dunia kwa constructions, na si kuboresha mali asili tuliyorithi, nawaza pale ambapo miji yote na vijiji vitakapokuwa vimeendelea sana na kufanana na new York city dunia itafananaje? Hapa namaanisha vijiji vyote ndani ya kigoma, singida, huko umasaini na dunia nzima vina matreni ya umeme, magorofa, magari ya kisasa n.k
Mji niliopo una joto kweli tofauti na miaka 30 iliyopita, kwa sababu ya maendeleo tumekata miti kweli, na ni kweli tuna maendeleo, magorofa, maji ya bomba, lami, nguzo za umeme.
zamani ilikuwa ukitembea unakutana na miti mikubwa ya asili,ndege wa aina mbalimbali, hewa nzuri na baridi. Sasa tuna lami, tunaendesha magari kwa raha, magorofa yenye lift na AC Ila Ile miti haipo tena, kuna aina flani ya ndege hawaonekani tena, hewa ina utofauti na hali ya hewa haitabiriki, kunaweza kukawa na joto na jua kali kupitiliza kitu ambacho hakikuwepo kabla.
Anyway sababu hii ndo tafsiri binadamu wote duniani tuliyoichagua ya maendeleo, tujipongeze kwa hatua tuliyopiga.
Moto ni mambo mkuu.Mambo ni motooo
Nenda kajinyonge wewe mzandiki.Wekeni umeme kwanza. Jengeni vituo vya kisasa ndiyo muanze matangazo.
Trillion 1.5 apewe lissu maana kawa omba omba.Hakuna cha kiwanda wala cha nini trilion 1.5 ipo mifukoni mwa wajanja wachache na bado wanaendelea kuitafuna Nchi kama mchwa
Wallah Majina huumba! Bwana Ushuzi umeandika Ushuzi.Hakuna cha kiwanda wala cha nini trilion 1.5 ipo mifukoni mwa wajanja wachache na bado wanaendelea kuitafuna Nchi kama mchwa
HIYO RELI YENU HAIWEZI KUNISAIDIA KUPATA CHAKULA WALA KUNIPELEKEA WATOTO WANGU SHULEHabari Njema kwa watanzania wote wapenda maendeleo.
Zoezi la Reli la utandikaji wa reli ya Standard Gauge (SGR) Sasa imeingia rasmi jijini Dar es Salaam na kwa sasa zoezi hilo linafanyika eneo la Vingunguti jijini hapa.
Naibu Waziri wa fedha amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo huku akisema mpaka sasa Serikali imeshatoa zaidi ya Trillion 2 kwenye mradi wa Reli ya SGR.
Kwa habari zaidi karibu katika youtube page ya TRC uone zaidi.
Alafu wewe ukute unapaki chombo chako cha usafiri CCM maana kwako sio salama.HIYO RELI YENU HAIWEZI KUNISAIDIA KUPATA CHAKULA WALA KUNIPELEKEA WATOTO WANGU SHULE
Habari Njema kwa watanzania wote wapenda maendeleo.
Zoezi la Reli la utandikaji wa reli ya Standard Gauge (SGR) Sasa imeingia rasmi jijini Dar es Salaam na kwa sasa zoezi hilo linafanyika eneo la Vingunguti jijini hapa.
Naibu Waziri wa fedha amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo huku akisema mpaka sasa Serikali imeshatoa zaidi ya Trillion 2 kwenye mradi wa Reli ya SGR.
Kwa habari zaidi karibu katika youtube page ya TRC uone zaidi.
Nakumbuka mwaka 2002 nilienda mkoa wa Kagera kwa gari ila nilienda huko kwa siku 2 tokea Dar, mara ya kwanza nililala SIngida na tukaenda lala Kahama..! Sikuhizi nasikia siku usiku mmoja tu Kahama siku ya pili unaingia Bk, Mikoa ya Lindi na Mtwara hapo nyuma walikuwa wanalala wakati ni Km 500+ lakini sikuhizi masaa 8 tu umefika Mtwara...! Sijui unawaza turudi huku ama vipi..!!
Mama yako anajua mimi siyo mzandiki. Muulize.Nenda kajinyonge wewe mzandiki.
Trillion 1.5 apewe lissu maana kawa omba omba.
Mama yangu ni wewe. Mzandiki mla Urojo we!Mama yako anajua mimi siyo mzandiki. Muulize.
Wengine wawe wanacheza Ngoma na kutwa kuisifia CCM halafu wengine wawachangie hela za maendeleo.Ni vyema watanzania tukaanzisha utamadini wa kuchangia majimbo yaliyo nyuma kimaendekeo, ifike siku bweni, shule au hospitali ikijengwa Singida mashariki au Simanjiro tusikie imejengwa kwa msaada wa wanajimbo wa Ukonga, Kibamba, Arusha, Ilala, Hai, Vunjo nk. Hii itakuwa tamaduni nzuri sana watanzania wenzangu.
Reli ni njia mmoja wapo ya usafiri,itasafirisha wewe,mwalimu,mwanafunzi askari,wagonjwa,madawa,daktari,mbolea,mkulima,mfanyabiashara,bidhaa mbali mbali,inakugusa upende usipende.HIYO RELI YENU HAIWEZI KUNISAIDIA KUPATA CHAKULA WALA KUNIPELEKEA WATOTO WANGU SHULE
TAZARA pia ilishika kasi Demokrasia na utawala wa Sheria ndio unatakiwa ushike kasi.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa dhati kukamilisha mradi mkubwa wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo tayari kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 2 kimetolewa mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi huo.
Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi eneo la Soga, umbali wa kilometa 53, na kujionea maendeleo makubwa ya ujenzi wa reli hiyo.
Ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wake na kumpongeza mkandarasi anaye jenga reli hiyo, Kampuni ya Yapi Merkezi, kwa kutekeleza ujenzi huo kwa viwango vya hali ya juu ambapo ameelezwa kuwa, treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro inatarajia kuanza safari zake Mwezi Novemba mwaka huu kama kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.
"Ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake kubwa na kuamua kwa dhati kutekeleza mradi huu mkubwa na miradi mingine, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, ambayo kukamilika kwake kutachochea uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Kijaji
"Tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, tutakuwa na viwanda kila mahali, tumeanza ujenzi wa mradi wa umeme wa megawat 2,115, viwanda vitazalisha bidhaa ambazo zitahitaji miundombinu ya usafirishaji, reli hii itatumika na tunatarajia ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa ni nchi yenye kipato cha kati" aliongeza Dkt. Kijaji
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo umekamilika kwa asilimia 42.
"Mradi wetu unaenda vizuri na kwa wakati, zoezi la ujenzi na utandikaji reli tumeanza katika Jijini la Dar es Salaam umeanza na unaendelea vizuri ambapo ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 55 na utandikaji wa reli katika Jiji hili utafikia kilometa 10 mwishoni mwa mwezi Februari" alifafanua Mhandisi Masanja.
na nguvu kubwa imeelekezwa katika ujenzi wa tuta na madaraja, zezi ambalo limefikia asilimia 55 hivi sasa" alifafanua Mhandisi Masanja
Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Mwanza, na baadae kuunganisha mtandao wake na nchi jirani za Kongo, Uganda, Burundi na Rwanda, unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 7.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezungumza na wakazi wa eneo la Guluka Kwalala, Gongo la Mboto, waliokuwa wakiendelea na taratibu zao za kulipwa fidia ambapo amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaletea maendeleo.
Baadhi ya wakazi hao, pamoja na kuiomba Wizara ya Ardhi na Makazi iwasaidie kupata viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao baada ya kulipwa fidia kupisha ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa, wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia ustawi na maendeleo ya nchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.