Pre GE2025 Ujenzi wa SGR Mwanza - Isaka wafikia 63%

Pre GE2025 Ujenzi wa SGR Mwanza - Isaka wafikia 63%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amelishauri Shirika la Reli Tanzania (TRC) kushughulikia changamoto zilizojitokeza katika ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam–Dodoma ili zisijirudie katika ujenzi wa kipande cha Mwanza–Isaka.

Prof. Mbarawa ametoa ushauri huo alipokuwa Malampaka, mkoani Simiyu, akikagua maendeleo ya mradi huo. Amesema ujenzi wa reli hiyo utafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa wakazi wa Simiyu, Mwanza na mikoa jirani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, amesema ujenzi wa kipande hicho umefikia asilimia 63.04 na TRC itahakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi wanufaike.

 
Back
Top Bottom