Ujenzi wa shimo la maji taka

Ujenzi wa shimo la maji taka

kemi2011

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2013
Posts
735
Reaction score
290
Naomba ushauri. Nimechimba shimo na kukutana na maji kwa kina cha futi tisa.

Nifanye nini wapendwa? Yaani nimekwama.
 
Naomba ushauri. Nimechimba shimo na kukutana na maji kwa kina cha futi tisa

Nifanye nini wapendwa? Yaani nimekwama
Achana na hilo shimo litakusumbua fanya mambo mengine
 
Kwa shimo la majitaka futi 9 linatosha urefu. Kama ni shimo la awali (septic) tafuta pump ya kuyatoa maji wakati unamwaga zege. Ili zege ishike mapema changanya na kemikali ya kugandisha zege kwa muda mfupi. Inapatikana madukani kama nabaki. Kama ni shimo la la mwisho (soak away) usiendelee kuchimba zaidi kama sehemu ina maji. Tafuta pump ya kuyatoa maji kwa mda wakati mafundi wanapanga tofali kuja juu.
 
Futi 9 inatosha mkuu.. kama ni lile la duara liongezee diameter tuu .
 
Tumieni hii hamtajuta, miaka 50 haijai haina service, nichekini 0784934147
IMG20201002084847.jpeg
IMG20201019153606.jpeg
IMG20200826091755.jpeg
 
Bio-digester septic tank,teknolojia mpya mjini kutoka kampuni ya Kenye Bioseptic
 
Naomba ushauri. Nimechimba shimo na kukutana na maji kwa kina cha futi tisa.

Nifanye nini wapendwa? Yaani nimekwama.

Futi tisa zinatosha. Ili kulinda mazingira, ni bora shimo hilo ukaliweka kwenye futi nane mwisho. Mimina zege kali chini. Pembeni weka matofali ya kuyalaza. Chapia kwa ndani, weka na niru. Hata tone moja la maji lisitoke nje kuingia ndani, wala la ndani lisitoke kwenda nje, isipokuwa kwenye majitaka yanayoingia na yatokayo tu.

Dizaini ya septiki tenki utakalojenga inabidi iboreshwe. Binafsi nimeshiriki kusanifu na kutekeleza maseptiki tenki bora na ya kisasa; ambapo wanafunzi walioyafanyia utafiti maabara, wameyakuta na ufanisi mkubwa kwenye kuondoa uchafu.

Maji yatokayo kwenye tenki, ukiyaangalia huwezi kuamini yanatoka kwenye septiki tenki. Rafiki yangu yeye alichukua dizaini hiyo na kuiboresha, na ambapo maji yatokayo kwenye septiki tenki ni safi kiasi kwamba anayatumia kumwagilizia bustani.

Mlenge.
 

Futi tisa zinatosha. Ili kulinda mazingira, ni bora shimo hilo ukaliweka kwenye futi nane mwisho. Mimina zege kali chini. Pembeni weka matofali ya kuyalaza. Chapia kwa ndani, weka na niru. Hata tone moja la maji lisitoke nje kuingia ndani, wala la ndani lisitoke kwenda nje, isipokuwa kwenye majitaka yanayoingia na yatokayo tu.

Dizaini ya septiki tenki utakalojenga inabidi iboreshwe. Binafsi nimeshiriki kusanifu na kutekeleza maseptiki tenki bora na ya kisasa; ambapo wanafunzi walioyafanyia utafiti maabara, wameyakuta na ufanisi mkubwa kwenye kuondoa uchafu. Maji yatokayo kwenye tenki, ukiyaangalia huwezi kuamini yanatoka kwenye septiki tenki. Rafiki yangu yeye alichukua dizaini hiyo na kuiboresha, na ambapo maji yatokayo kwenye septiki tenki ni safi kiasi kwamba anayatumia kumwagilizia bustani.

Mlenge.
Hizo septic zinadizain gani mkuu unatia na bacteria/enzyme?
 
Back
Top Bottom