Futi tisa zinatosha. Ili kulinda mazingira, ni bora shimo hilo ukaliweka kwenye futi nane mwisho. Mimina zege kali chini. Pembeni weka matofali ya kuyalaza. Chapia kwa ndani, weka na niru. Hata tone moja la maji lisitoke nje kuingia ndani, wala la ndani lisitoke kwenda nje, isipokuwa kwenye majitaka yanayoingia na yatokayo tu.
Dizaini ya septiki tenki utakalojenga inabidi iboreshwe. Binafsi nimeshiriki kusanifu na kutekeleza maseptiki tenki bora na ya kisasa; ambapo wanafunzi walioyafanyia utafiti maabara, wameyakuta na ufanisi mkubwa kwenye kuondoa uchafu. Maji yatokayo kwenye tenki, ukiyaangalia huwezi kuamini yanatoka kwenye septiki tenki. Rafiki yangu yeye alichukua dizaini hiyo na kuiboresha, na ambapo maji yatokayo kwenye septiki tenki ni safi kiasi kwamba anayatumia kumwagilizia bustani.
Mlenge.