KERO Ujenzi wa soko kila Wilaya Pemba ni jambo zuri lakini msibomoe magenge kando ya barabarani, yanatusaidia

KERO Ujenzi wa soko kila Wilaya Pemba ni jambo zuri lakini msibomoe magenge kando ya barabarani, yanatusaidia

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Sisi Wakazi wa Pemba kuna jambo limekuwa likitutesa kwa muda na kutuathiri sana sisi Wananchi wa eneo hili.

Miaka ya hivi karibuni Serikali imekuwa ikijenga masoko ya kisasa katika kila Wilaya huku Pemba, kwa mfano hapa Chakechake kuna soko lipo pale Matemani.

Pamoja na faida na uzuri wa masoko hayo yanayojengwa upande mwingine yamekuwa ni mwiba mkali kwetu, kwani Serikali imekuwa ikibomoa magenge na sehemu ambazo tumekuwa tukinunua mahitaji yetu ya kila siku, lengo lao ni kulazimisha Wananchi tukanunue mahitaji yetu kwenye haya masoko.

Kwa miezi miwili mitatu iliyopita magenge na maduka yaliyopo barabarani yamevunjwa kwa maagizo ya Halmashauri.

Wananchi kutoka maeneo kama Mkoroshoni, Gombani na maeneo mengine kote huko wamevunjiwa maduka na magenge ili waende kwenye hilo soko kuu kununua mahitaji yao.

Ieleweka wazi kuwa sio kwamba sisi Wananchi hatupendi masoko mapya kwenye Wilaya, HAPANA, lakini mpaka kufika huko ni gharama kubwa maana ni lazima upande Bajaji au usafiri mwingine wowote kwenda kwenye soko.

Kuna soko liko pale Tumbe kwa hiyo maeneo yote karibu na Tumbe wamebomoa magenge ili kufanya Wananchi waende kwenye hilo soko.

Muda mwingine unakuta mtu umeamka na Shilingi 1,000 na unataka ununue zako tungure (nyanya) na viungo ili utengeneze mchuzi lakini huwezi kufanya hivyo kwa hiyo Sh 1,000, ndio utatumia kama nauli ya kufika huko soko kuu.

Tunaomba Serikali iliangalie hili hasa Watu wa Halmashauri, sio kila siku mtu anaweza kwenda sokoni. Tunaomba mruhusu magenge na maduka barabarani ili tupate mahitaji yetu kwa urahisi.
 
Aliyekwambia serikali inataka upate mahitaji yako kirahisi nani?
Pale michakaiñi kuña mahitaji gani muhimu?
Hàkuna wateja na hadi sasa hawalipi kodi!
Hasara tupu.
#HatunaMbadala2025
 
Aliyekwambia serikali inataka upate mahitaji yako kirahisi nani?
Pale michakaiñi kuña mahitaji gani muhimu?
Hàkuna wateja na hadi sasa hawalipi kodi!
Hasara tupu.
#HatunaMbadala2025
Nimefikiria sana kuwa inakuwaje wapanga miji wa serikali hawakulijua suala la wazi kama hili?
 
Nimefikiria sana kuwa inakuwaje wapanga miji wa serikali hawakulijua suala la wazi kama hili?
Wanavyogombania tenda za kujenga unafikiri nani atatumia akili kufikiri? Wote wanawaza watapata mgao kiasi gani, machinga hata mpige kelele kwamba hilo eneo halifai hakuna wa kusikiliza.
Ebu ona pale chakechake michakaini wànataka kulazimisha gari za abiria ziingie kule bondeni ili zilipe ushuru!
 
Back
Top Bottom