Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WIZARA YA TAMISEMI INAKUSAIDIA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA STENDI YA HALMASHAURI YA MOMBA
Katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe aliuliza swali lililojibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Deo Ndejembi
"Halmashauli ya Wilaya ya Momba ni miongoni mwa Halmashauli 56 ambazo zimewekwa kwenye kundi ambalo tutapangiwa fedha za maendeleo asilimia 20. Je, ni upi mkakati wa TAMISEMI kutujengea Stendi kwenye Kata ya Kamsamba Ukanda wa chini, Kata ya Ikana Ukanda wa Juu kwasababu sehemu zote hizi zinaunganisha Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Rukwa na kuna uhitaji mkubwa sana wa Stendi ili zitumike kama chanzo cha Mapato kwenye Halmashauri? - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
"Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Sichalwe, amekuwa akilifuatilia sana hili na amekuwa akija mara kadhaa Ofisi ya Rais TAMISEMI. Tutaendelea kutenga fedha kadiri ya upatikanaji wake ili tuweze kuwajengea wananchi wa Momba Stendi hizi na kuiwezesha Halmashauli ya Momba kuwa na uwezo wa kupata fedha ya mapato kutokana na miradi hii" - Mhe. Deo Ndejembi (Mb), Naibu Waziri TAMISEMI