Ujenzi wa stendi ya kisasa umeanza?

Ujenzi wa stendi ya kisasa umeanza?

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Ujenzi wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani ktk eneo la Mbezi mwisho jijini dsm ulitakiwa kuanza mwezi huu wa Julai kwa mujibu wa kauli ya uongozi wa jiji iliyotolewa mwaka jana, je ujenzi huo umeanza au umeahirishwa?

Sababu iliyo nisukuma kujua jambo hilo ni kutokana na usumbufu mkubwa uliopo ktk stendi ya ubungo, msongamano n.k.

Sina hakika lkn kulikuwa na mvutano wapi haswa stendi hiyo ijengwe, mbezi mwisho au luguruni/kibamba, hii ni kutokana na eneo la mbezi kuwa finyu nk, je muafaka umepatikana?

Tunafahamu kuwa stendi ya mabasi ya mikoani na nchi jirani ni chanzo kikubwa cha mapato ya nchi yetu haswa ktk jiji la Dsm hiyo ni muhimu mamlaka husika ziharakishe ujenzi wa stendi hiyo na ijengwe mahali panapo faa kwa muda mrefu.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Tunasubiri ripoti ya tatu ya makinikia itakayoongozwa na pro Lipumba na kundi lake la Mungiki

from Katesh using Siemens C55
 
Kweli ni jambo la muhimu ktk uchumi wa nchi yetu, kama ilivyo bandari na viwanja vya ndege n.k.

Kwa Jiji la DSM ambalo linalopokea wageni wengi kutoka mikoani na nchi jirani ni lazima kituo kiwe kikubwa na cha kisasa.
 
Huwezi kuwakuta watukanaji kwenye thread kama hii kwa sababu Halmashauri ya jiji ni ya Chadema.
 
maendeleo hayana chama, sote tunahitaji maendeleo kwa faida yetu na vizazi vyetu.
 
Back
Top Bottom