Husika na mada tajwa hapo juu,
Kimsingi eneo linalosemekana limeandaliwa kwa ajili ya stend ya mabasi ya mwendo kasi kwa maeneo ya gongolamboto, sidhani kama lipo mahali sahihi.
Wahusika waliangalie hili jambo kwa umakini kusiwe na upigaji wa kipekee kwa maana kule Pugu stesheni , stend ilishakamilika na ipo tayari kwa matumizi.
Kutoka gongolamboto hadi pugu stesheni kuna tofauti ya wastani wa kilometa 4, wastani wa mafuta ya nusu lita hadi lita moja kwa mabasi ya diesel.
Wahusika tunaomba mradi huu ufike stesheni badala ya kuishia Gongo la Mboto.
Nawasilisha