Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama nguzo atatumia tofali,aongeze idadi.120m x 80m, hizi ni eka 2 na chenchi juu, hii ni estates sio kiwanja, hongera. Tafuta fundi akufanyie proper estimates ila unaweza kupata mwanga kidogo hapa.
Jumla ya mzunguko- 400m
Urefu wa tofali moja - 0.48m
No ya tofali kwa kila kozi - 400/0.48 = 833.3 tofali.
Msingi avarage kozi 5 za tofali za 6” - 833.3 x 5 = 4167 tofali
Juu avarage kozi 8 za tofali za 5” - 833.3 x 8 = 6666 tofali.
Jumla tofali za 6”ni 4167 na za 5” ni 6666, hii ni rough estimate, ila fundi anaweza kukupa kilicho bora zaidi kutokana na nature ya eneo lako.