benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Serikali ya Tanzania imesema iko katika hatua za mwisho za majadiliano na Serikali ya Vietnam kujenga viwanda vitakavyobangua Korosho hapa nchini (Tanzania) ili kuiongezea thamani badala ya kuiuza ikiwa ghafi kama inavyofanyika kwa kiasi kikubwa hivi sasa.
Taarifa kutoka Kituo cha uwekezaji nchini (TIC) iliyotolewa. wakati wa Kongamano la Uchumi kati ya Tanzania na Vietnam imefafanua kuwa, Vietnam ambayo imekuwa miongoni mwa vinara kati ya wanunuzi wakuu wa Korosho ya Tanzania imekubali kuanzisha viwanda hivyo hapa nchini kwa kushirikiana na wawekezaji binafsi wa ndani.
Ikumbukwe kuwa Vietnam ndiye mnunuzi mkubwa zaidi wa Korosho yetu akifuatiwa na India ambao kwa pamoja wananunua karibu ya aslimia 90 ya Korosho yote ya Tanzania.
Hii ni habari njema kwa Wakulima wa Korosho lakini pia kwa watanzania wengi ambao watanufaika katika mnyororo mzima wa thamani katika uwekezaji huu, kuanzia wakati wa ujenzi mpaka viwanda utakapokamilika.
Rekodi zinaonesha kuwa Vietnam ina miradi michache tu hapa nchini (MIradi Sita) iliyosajiliwa na TIC lakini miradi hii ina thamani kubwa inayofikia Dola za Kimarekani Bilioni 1.57 ambayo imezalisha zaidi ya Ajira 200,000 kwa Watanzania
.