Katika mijadala mingi na mikutano ya Viongozi na wafuasi wa ccm,wamekuwa wakitolea mifano eti wamefanya maendeleo katika elimu na miundo mbinu ya barabara hivyo kuwataka wananchi waendelee kuwaamini.Kwa wasiojua kutathmini kwa kina na wanaotumia WINGI(quantity) badala ya UBORA(quality) wanaweza kuamini hayo.Kumbe ni changa la macho na kuongeza ugumu wa maisha na kongwa la mzigo mzito kwa mwananchi.
HEBU JIULIZE KATIKA SUALA LA ELIMU
Serikali ilipunguza ada ya kusoma sekondari kwa 50%, mfano o-level toka 40,000/= mpaka 20,000/= kwa mwaka.Kwa kufanya hivyo waliamua kurudisha gharama zote kwa mwananchi na hivyo kumwongezea mzigo zaidi wa ule wa awli.Mfano;
-wananchi wanajenga madarasa,ofisi,vyoo n.k
-wanapeleka madawati,karatasi(rimu),wanalipa ada ya mtihani,wanalipa taaluma,wanalipa walimu wa kujitolea,wanalipa walinzi wa shule n.k.gharama ya vyote hivyo ni zaidi ya mara 5 ya kulipa elfu 40 za awali.Kwa mtu anayejua siri hiyo atawaona kama wachekeshaji na wacheza komedia.
SUALA LA UJENZI WA BARABARA
Tunapozungumza ujenzi wa miundombinu ya barabara,ni sharti kuhusianisha na namna barabara hizo zinavyopunguza ugumu na makali ya maisha kwa mtanzania wa hali ya chini na wala si kwa wenye magari kupita kwa uraisi.Ni sawa mwaka 2005 hadi 2012 kuna urefu wa zaidi ya km 12,000 za barabara za lami nchini.JE,barabara hizo zimefanya yafuatayo ? -zimepunguza kwa kiasi gani nauli au zimeongeza?
-zimepunguza gharama za usafirishaji wa vifaa vya ujenzi,chakula,pembejeo za kilimo n.k kwa
kiasi gani au zimeongeza zaidi?
Haya maswali ndio ya kuwauliza hawa viongozi na vigogo ccm na kwa hakika wanapaswa kutoa majibu yenye mantiki na sio ya kisiasa.Kujisafisha kwao ni bure kama haya hayagusi maisha ya mwananchi wa kawaida na sio hoja za msingi kutumika kama kishawishi kwa watanzania wa karne ya 21.MAANA HOJA YA MSINGI LAZIMA IBAKI KUWA CCM IMEWEZAJE KUPUNGUZA UMASKINI WA MTU MMOJA MMOJA NA KUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA KWA UJENZI WA SHULE NA BARABARA.Katika hayo ndiyo wananchi wataona kuwa wanapumbazwi au la ! SEMENI NA WENGINE JAMANI.​