ujenzi was shule na barabara katu si hoja ya msingi ya kuwashawishi wananchi kuikubali CCM-2015

ujenzi was shule na barabara katu si hoja ya msingi ya kuwashawishi wananchi kuikubali CCM-2015

PGMMKOMA

Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
26
Reaction score
7
Katika mijadala mingi na mikutano ya Viongozi na wafuasi wa ccm,wamekuwa wakitolea mifano eti wamefanya maendeleo katika elimu na miundo mbinu ya barabara hivyo kuwataka wananchi waendelee kuwaamini.Kwa wasiojua kutathmini kwa kina na wanaotumia WINGI(quantity) badala ya UBORA(quality) wanaweza kuamini hayo.Kumbe ni changa la macho na kuongeza ugumu wa maisha na kongwa la mzigo mzito kwa mwananchi.
HEBU JIULIZE KATIKA SUALA LA ELIMU


Serikali ilipunguza ada ya kusoma sekondari kwa 50%, mfano o-level toka 40,000/= mpaka 20,000/= kwa mwaka.Kwa kufanya hivyo waliamua kurudisha gharama zote kwa mwananchi na hivyo kumwongezea mzigo zaidi wa ule wa awli.Mfano;
-wananchi wanajenga madarasa,ofisi,vyoo n.k
-wanapeleka madawati,karatasi(rimu),wanalipa ada ya mtihani,wanalipa taaluma,wanalipa walimu wa kujitolea,wanalipa walinzi wa shule n.k.gharama ya vyote hivyo ni zaidi ya mara 5 ya kulipa elfu 40 za awali.Kwa mtu anayejua siri hiyo atawaona kama wachekeshaji na wacheza komedia.
SUALA LA UJENZI WA BARABARA
Tunapozungumza ujenzi wa miundombinu ya barabara,ni sharti kuhusianisha na namna barabara hizo zinavyopunguza ugumu na makali ya maisha kwa mtanzania wa hali ya chini na wala si kwa wenye magari kupita kwa uraisi.Ni sawa mwaka 2005 hadi 2012 kuna urefu wa zaidi ya km 12,000 za barabara za lami nchini.JE,barabara hizo zimefanya yafuatayo ? -zimepunguza kwa kiasi gani nauli au zimeongeza?
-zimepunguza gharama za usafirishaji wa vifaa vya ujenzi,chakula,pembejeo za kilimo n.k kwa
kiasi gani au zimeongeza zaidi?

Haya maswali ndio ya kuwauliza hawa viongozi na vigogo ccm na kwa hakika wanapaswa kutoa majibu yenye mantiki na sio ya kisiasa.Kujisafisha kwao ni bure kama haya hayagusi maisha ya mwananchi wa kawaida na sio hoja za msingi kutumika kama kishawishi kwa watanzania wa karne ya 21.MAANA HOJA YA MSINGI LAZIMA IBAKI KUWA CCM IMEWEZAJE KUPUNGUZA UMASKINI WA MTU MMOJA MMOJA NA KUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA KWA UJENZI WA SHULE NA BARABARA.Katika hayo ndiyo wananchi wataona kuwa wanapumbazwi au la ! SEMENI NA WENGINE JAMANI.
 
Mh!!!! PGMKOMA wewe ni kiboko. Halafu wewe ni mbumbumbu wa kutisha. Hizi ni fikra za CDM ambazo zimejengwa kwenye falsafa ya NIHILISM. Yaani huoni manufaa ya barabara wala kuongezeka kwa watoto wanaokwenda shule?
  • La msingi, kazi ya serikali ni kujenga miundombinu mbalimbali ya kiuchumi itakayomwezesha mwananchi kufanya shughuli zake za kiuchumi kwa urahisi. barabara ni mojawapo ya miundo mbinu hiyo. Zinapokwepo barabara mzuri zinakuwa kichocheo cha maendeleo ya mtu mmoja mmoja. huoni mahindi yalivyojaa Rukwa huku sehemu nyingine za nchi zina njaa?
  • Hongera serikali mpango wa sekondary za kata hatimaye unaonyesha mafanikio makubwa mno. Enrollment ya FORM V mwaka jana ilitawaliwa na vijana waliotoka sekondari za kata BRAVO serikali. Kilichobaki ni kidogo tu ambacho chini ya kamanda Kikwete atakimaliza sasa hivi nacho ni KUJAZA WAALIMU KATIKA SHULE HIZO NA HATIMAYE MISSION ACCOMPLISHED.
Wacha STEREOTYPE za ajabu wewe.
 
Wananchi tuna taabu kubwa sana. Tunalipishwa michango kila leo, tunalipa kodi kwenye kila bidhaa, tunakatwa mishahara yetu, ukiwa na kabiashara wanakukamua, omba uwe na ndugu tra. Aafu baadaye waliokuwa wanakula kodi zetu bila kukatwa wanakuja kujigamba wamejenga wao!!..? Kuna wakati huwa naamini kama Mungu ametuzibia masikio ili kutosikiliza kelele zetu kwani tunajitakia wenyewe.
 
Acheni umbumbumbu,kwa nini hamtaki kukubali kuwa CCM haina nia nzuri na watanzania? wewe unasema watoto wengi wanaenda kidato cha V,unafikiri wengi wao wanatoka shule zipi kama sio za BINAFSI.
Sikiliza mfano TARAFA moja ya wilaya ya iramba mwaka 2011 ilikuwa na wanafunzi 318 toka shule 5 za kata hiyo,kati ya hao wote waliopata daraja (division) I_III ni wanafunzi 11 tu ambao ndio wanaweza kuchaguliwa kwenda kidato cha tano (5).Inamaana wanafunzi 307 wote wapo nyumbani au baadhi eti ualimu.

Yapo mambo yasiohitaji siasa ndugu,kwani madhara yasipo kupata wewe yatawapata ndugu zako au rafiki zako wa karibu kabisa.KUMBUKA KUCHAGUA KIONGOZI NI HIARI,LAKINI MADHARA YA KIONGOZI HUYO MBOVU HUTACHAGUA, ndio maana wote wa na ccm pia pamoja na ushabiki wao wa kushabikia ccm,madhara yanawapata tu.

MASUALA YA MSINGI NI HAYA BARABARA ZIMEPUNGUZAJE MAKALI YA MAISHA NA UGUMU WA MAISHA KWA MWANANCHI MMOJA MMOJA? NA KAZI YA SERIKALI NI NINI KATIKA ELIMU MAANA GHARAMA ZOTE ZIPO KWA MWANANCHI ?
 
Back
Top Bottom