Kunapokuwa na foleni nchini Ujerumani, madereva hulazimika kisheria kupita pembeni ya barabara ili kuacha nafasi ya magari ya dharura kama magari ya wagonjwa na zimamoto.
Je unadhani ni muhimu kwa nchi nyingine kufuata utaratibu huu?
Na hizi barabara zetu kama kichochoro utatanuaje uache nafasi ya ambulance. Huo ukingo uanaongelea kuna wamachinga wamepanga nyanya zao na wanajiona wapo sahihi kabisa. Bila kusahau wazee wa haraka daladala wanaojiona daima wana haki ya kutanua.
Hujakaa sawa unakutana na gari la jeshi au FFU wakiona foleni wanatanua upande sio wao.
Kabla ya kutoa hiyo elimu, watengeneze barabara kwanza.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.