Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Sisi kama Watanzania na tume yetu Huru ya uchaguzi kuna jambo la kujifunza.
Ujerumani ni nchi ya watu mil 83, wamefanya uchaguzi mkuu jana uliokuwa na ushindani mkubwa sana na ukifuatiliwa ulimwenguni kote.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Inasemekana masaa nane baada ya uchaguzi, wameshamaliza zoezi la kuhesabu kura na matokeo ya awali yametoka, matokeo ambayo huwa hayatofautiani pakubwa na matokeo rasmi. Tume yetu Huru ya Uchaguzi iige mfano huu, matokeo yajulikane mapema na siyo hadi kutokee mivutano ndipo yatangazwe hasa yale ya wabunge na madiwani.
===
Ufuatiliaji wa JamiiCheck

JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini kuwa ni ya kweli. Nchini Ujerumani vituo vya kupigia kura hufunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni na kisha zoezi la kuhesabu kura huanza mara moja katika vituo husika mara baada ya vituo kufungwa.
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa shirikisho, Ujerumani kwa mwaka 2025 yalitangazwa usiku wa Februari 24, 2025 saa chache baada ya kufungwa kwa vituo vya kuhesabia kura jioni ya tarehe 23, Februari 2025.
Kwa mujibu wa Afisa msimamizi wa uchaguzi wa shirikisho, Ujerumani walitoa taarifa kwa vyombo vya habari usiku kwa mara ya kwanza saa 7:15 usiku. Kisha wakatoa tena maboresho saa 10:10 usiku (alfajiri). Matokeo yalikusanywa kwa mawasiliano ya njia ya simu na njia nyingine za kielektroniki kutoka katika kila kituo cha kupigia kura.
Taarifa ya Afisa msimamizi wa uchaguzi wa shirikisho inaeleza kuwa matokeo rasmi yatatangazwa baadae na tume ya uchaguzi ya shirikisho Machi 14, 2025 katika kikao cha wazi cha bunge (Bundestag) huko Berlin.