Pre GE2025 Ujerumani: Nchi ya watu Milioni 83 inasemekana wamemaliza kuhesabu kura ndani ya saa 8 baada ya kukamilisha kwa zoezi, Tanzania tuna la kujifunza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kumbuka na hawaja gawa mikoa wakati wa kampeni kwaajili ya kusaidia Chama flani. Kuiga huko labda jua libadili mwenendo aisee.
 
Kuhalalisha haramu ni kazi ngumu sana!
Kuibiwa kura unatakiwa kuthibitisha kituo kipi uliibiwa huwezi ibuka tu kama nwehu oooh tunaibiwa kura

Kura zikipigwa onyesha vituo ulivyoibiwa na kama huyo wakala wako alilala usingizi au hadi kura zinaibiwa kituo alichosimamia na kama hivyo vituo unasema kura uliibiwa je hizo kura ni material kuweza kufanya matokeo ya uchaguzi yakibadilika kwa hizo za hicho kituo utashinda uchaguzi wa Raisi mbunge au diwani?

Mahakama itatumia hoja ya materiality principle kuamua hiyo kesi

Ukisema umeibiwa kura taja na kituo cha kura na ushahidi sio kubweka tu kama mbweha
 
Kumbuka Kuna nchi zinazofanya uchaguzi wa viongozi na Kuna wanao kamilisha ratiba ya uchaguzi. hizi ni nchi mbili tofauti ndio maana ata taratibu zao ni tofauti wengne wana midaharo wengne hawawezi kujaribu kabisa.
 
Ndugu yangu Kuilinganisha Ujerumani na sisi mbona ni tofauti kubwa hivyo.

Wale wapi kidemokrasia zaidi sisi tupo chini ya mwavuli wa kijamaa.
 
Wewe hapo nyumbani kwako una chochote cha kujivunia?

German is a developed country and a digital one

Wewe na mimi tuko social media a


And we expect miracles
 
Tanzania haina mfano, maana hata leo ukiomba matokeo ya uchaguzi wa october 2025 wanakupa yamesha kamilika, wanajua nani atashinda na asilimia zake.

Mnapoteza muda kujadili vitu kama hivi Tanzania.
 
Wewe hapo nyumbani kwako una chochote cha kujivunia?

German is a developed country and a digital one

Wewe na mimi tuko social media a


And we expect miracles
Nyumbani kwangu na matokeo ya uchaguzi yanahusiana nini? Au ndiyo lazima ucomment ili na wewe urefushe uzi?
 
Na uchaguzi wao hakuna anayelalamika kuibiwa kura au kufanyiwa hujuma
 
Na uchaguzi wao hakuna anayelalamika kuibiwa kura au kufanyiwa hujuma
Kabisa maana sauti na maoni ya watu yanaheshimiwa, viongozi wanachaguliwa kutokana na matakwa ya Nchi sio kwa matakwa ya kikundi flani. Nzuri zaidi hakuna chawa ni kiongozi kutangaza Sera na zikikubalika wananchi wanafanya maamuzi, maisha yanaednelea bila msuko suko wowote.
 

Wapiga kura ni wangapi?
Ni asilimia ngapi ya waliojiandikisha?
 
JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini kuwa ni ya kweli. Nchini Ujerumani vituo vya kupigia kura hufunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni na kisha zoezi la kuhesabu kura huanza mara moja katika vituo husika mara baada ya vituo kufungwa.

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa shirikisho, Ujerumani kwa mwaka 2025 yalitangazwa usiku wa Februari 24, 2025 saa chache baada ya kufungwa kwa vituo vya kuhesabia kura jioni ya tarehe 23, Februari 2025.

Kwa mujibu wa Afisa msimamizi wa uchaguzi wa shirikisho, Ujerumani walitoa taarifa kwa vyombo vya habari usiku kwa mara ya kwanza saa 7:15 usiku. Kisha wakatoa tena maboresho saa 10:10 usiku (alfajiri). Matokeo yalikusanywa kwa mawasiliano ya njia ya simu na njia nyingine za kielektroniki kutoka katika kila kituo cha kupigia kura.

Taarifa ya Afisa msimamizi wa uchaguzi wa shirikisho inaeleza kuwa matokeo rasmi yatatangazwa baadae na tume ya uchaguzi ya shirikisho Machi 14, 2025 katika kikao cha wazi cha bunge (Bundestag) huko Berlin.
 
Nadhani wao wako mbali kwa teknolojia ikilinganishwa nasi Africa,,wenzetu walikuwa na maisha tuliyo nayo sasa Zapata karne 6 na kuendelea. Lujilinganisha nao ni kutuonea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…