Mimi naona maelezo yaliyopatikana ni ya pande mbili,yaani Lulu na Sethi.Lakini sikuona sababu ya lulu kuondoka eneo la tukio mapema kiasi hicho kwasababu mtu aliyokuwa anamuogopa tayari alikuwa hana fahamu.Angesubiri mpaka daktari aje waondoke na mwili mpaka hospitari.
Tatizo hapa ni kwanini alitoweka eneo la tukio mapema kiasi hiki,kitendo hicho ndicho kinapelekea wadau wahisi kama pengine alihusika.
Mdogo wa marehemu yaani Sethi,amenukuliwa akisema alisikia sauti za malumbano, lakini alishindwa kuingia ndani kwasababu mlango wa chumbani ulikuwa umefungwa.Kwa mujibu wa kauli hii inaonyesha kuwa sauti zilizokuwa zinasikika zilikuwa za kawaida kiasi kwamba hazikumfanya apige keleke kuomba msaada kutoka nje.
Mtazamo wangu ni kwamba kama Marehemu angekuwa hai angetoa maelezo ya makovu yaliyokutwa kwa lulu kuwa yametokana na kipigo kutoka kwake au alikuja nayo; Lakini kama Lulu ndiye aliyetoa taarifa kwa Sethi kuhusu kudondoka kwa Kanumba,Basi hata Sethi anaweza kutoa ushuda wake kwa namna alivyo muona Lulu pindi alipompa taarifa, kwamba alimuona ana makovu au laa.
Ushauri wangu ni kwamba, hakuna tukio lisilokosa sababu,na ajali haina kinga; Fundisho hapa tuwe na kiasi kwa kila jambo:Simu za mkononi ni nzuri kama zitatumika kwa uaangalifu mkubwa,lakini ni mbaya kama zitatumika vibaya. Mimi naamini hakuna mpenzi asiye na wivu kwa mwinzi wake hasa kama anampenda, cha msingi tuwe makini na hivi vilonga longa