UJINGA: JANGA LINALOWATESA MASHABIKI MAN UNITED

UJINGA: JANGA LINALOWATESA MASHABIKI MAN UNITED

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Washabiki wa soka wana hisia kali sana, yaan si ajabu ukashangaa kuona mtu presha inapanda mpaka ana zirai, wengine wanakuwa wana furaha mpaka wanaishia kufanya vituko uwanjani, pia kuna wakina Steve, aliyekuwa mshabiki wa Young Africans na baadae kuhamia Azam, hawa hawafichi hisia zao yaani kutoa machozi kwao ni jambo la kawaida kabisa.
Mapenzi aliyokuwa nayo Haji Manara kwa Simba SC, ni ya ajabu sana. Ukiachana na ukweli kwamba amezaliwa katika familia ya wanajangwani, lakini huyu mtu anaweza kukana familia yake kwa ajili ya Sunderland ya Kariakoo. Angalia timu ya Simba baada ya kutolewa na UD Songo, eti Haji anasema yupo tayari kuwajibishwa kwa matokeo Simba wamepata; yaani huyu bwana anaipenda Simba mpaka washabiki wa upande wa pili huko jangwani wanaona wivu.
Msemaji wa Simba, Haji Manara
Huko Ulaya pia, washabiki wanapenda sana timu zao. Yaan Chelsea ya Super Frank, imecheza mechi tatu tu, lakini washabiki wameshasahau mazuri ambayo Frank katika kipindi anacheza soka ameyafanya ndani ya klabu ya Chelsea, washabiki eti wameandika mabango makubwa eti “Frank out.”
Moja ya jumbe za mashabiki wa Chelsee wakingoja kocha Frank Lampard (pichani) atimuliwe
Ukija huku kwingine, unaweza ukaona masihara eti Christiano Ronaldo, yale maajabu, ile migoli pamoja na damu aliyomwaga pale Santiago Bernabeu, Madrid, kiwango chake kikidondoka tu kidogo, washabiki wanamzomea. Cristiano, alijitahidi sana kuvumilia mpaka pale yalipomshinda na kuamua kutimkia Turin ambapo walimuonyesha mahaba hata pale alipowaondosha kwenye michuano ya klabu bingwa na kuwanyima nafasi ya kushangilia kombe ambalo wamelisubiri kwa zaidi ya miaka 24: kombe la ligi ya mabingwa Ulaya.
Christiano Ronaldo
Achana na yote hayo, hivi sasa klabu ya Barcelona na jeuri yao wanayosemaga kuwa wao ni zaidi ya klabu, leo hii wanapambana sana kumrudisha Neymar Jr, mchezaji ambaye aliwakana mchana kweupe na kudai hana furaha na maisha ya Camp Nou. Hata alipoondoka klabuni hapo, Neymar alionekana kujutia maamuzi aliyofanya. Mara kadhaa alionekana kurudi katika uwanja wa Camp Nou, alipoonekana kuanzia wachezaji mpaka washabiki walimkumbatia kama mtoto waliyemlea lakini ni wazi kabisa, Neymar ni mchezaji ambaye maisha yake ya soka yalianzia katika viunga vya klabu ya Santos huko nchini Brazil, mpaka pale Barca walipomuona na kumsajili kwa bei kubwa mno.
Neymar
Washabiki wa soka wamekuwa na njia nyingi sana za kuwakilisha maoni yao. Mfano, wakiwa uwanjani kama hawajapendezwa na jambo flani utawaona wanazomea, wakipendezwa hushangilia sana, kuna wengine wanaingia mpaka uwanjani ili hali wanajua ni makosa kufanya hivyo.
Lakini kuna njia nyingine washabiki wanayoitumia hivi sasa imekuwa maaarufu sana: mitandao ya kijamii. Katika mitandao ya kijamii hususani
Twitter, washabiki wamekuwa wanawasilisha maoni yao moja kwa moja kwa muhusika. Mfano, huko Ulaya, imekuwa ni kama sheria kwa mchezaji kuwa na akaunti Twitter. Ijapo siyo lazima kuwa na akaunti, lakini wachezaji wameshauriwa kufanya hivyo kwasababu, wanatakiwa kuwa karibu na mashabiki wao na njia pekee siyo kwa wao kushinda nao vijiweni bali huko mitandaoni ndio imekuwa vijiwe vya wachezaji na mashabiki wao.
Soka ni mchezo wa kiungwana; ndio maana katika sheria zake, sheria ya kwanza kabisa inasema,
“My game is fair play” yaani mchezo wangu ni wa kiungwana. FIFA kila mwaka inaendesha kampeni mbalimbali ili kuhakikisha soka unakuwa ni mchezo ambao unaunganisha binadamu wote duniani ukiachana na vikwazo kama, mipaka, rangi, dini, makabila na utaifa. Ile kampeni ya FIFA: “Say no to Racism” imeendelea kuendeshwa na shirikisho hilo kubwa zaidi la soka duniani miaka kenda.
Mojawapo ya posti zinazombagua Rashford kupitia mtandao wa Twitter
Viwanjani hivi sasa, mashabiki wanajua kabisa ukikutwa na kosa la kubagua mtu awe ni mshabiki mwenzio, mchezaji au yeyote yule, kwanza unafungiwa kushabikia soka maisha yako yote na; pia, kwa kuwa ni kosa la jinai, basi wanachofanya ni kukikabidhi kwa mamlaka husika ili wakushughulikie kulingana na sheria za nchi husika.
Lakini sasa, wale washabiki washamba, chuki zao hivi sasa wameziamishia katika mitandao ya kijamii kama Twitter, kwasababu wanaamini waanzilishi wa mitandao hii wana sera zinazolinda watumiaji wa mitandao hii (user/policy agreement).
Nimeshangazwa sana na klabu ya Manchester United kwa kufumbia macho vitendo vya ubaguzi wa rangi vinavyofanywa na washabiki wake dhidi ya wachezaji wa klabu hiyo. Tangu ligi kuu ya England (EPL) ianze, hii ni wiki ya tatu tu. Lakini mpaka sasa klabu ya Man U imeshapata mikwaju ya penati mitatu, katika hiyo mitatu, wameshakosa miwili. Kukosa kwa mikwaju hiyo kumepelekea klabu hiyo kupoteza point 5 yaan kipigo walichopata dhidi ya Crystal Palace na droo dhidi ya Wolves.
Marcus Rashford na Paul Pogba
Washabiki wa United wenye hasira zao, wameamua kuwabagua rangi wachezaji waliokosa mikwaju ile eti kwasababu wana asili ya Afrika. Marcus Rashford, katika wiki ya pili mfululizo anakuwa mhanga wa ubaguzi wa rangi baada ya Paul Pogba kubaguliwa eti kwasababu wamekosa mkwaju wa penati uliowanyima point tatu dhidi ya Wolves na Crystal Palace.
Eti, wanadai wachezaji hao kupata nafasi kucheza United ni bahati kubwa sana maishani mwao; lakini wao badala ya kupambana wao wanalegeza. Kwa hili wanaweza kuwa sawa mtu yeyote yule atakayepata nafasi kucheza klabu kama Man U, hiyo ni bahati lakini mashabiki hawa wanadai wachezaji wenye rangi kama ya Pogba na Rashford kuwepo ndani ya klabu ya United ni bahati wanamaanisha nini? Yawezekana pia hata mashabiki wenye rangi kama ya Pogba na Rashford kushabikia klabu kama Man U pia ni bahati hivyo kuweni makini.
Uongozi wa mtandao wa Twitter umekutana na baadhi ya viongozi wa Man U, ili kuhakikisha vitendo kama hivi havijirudii ndani ya mtandao huu. Kwa mantiki hii Twitter inaenda kuwa kama Old Trafford, mshabiki yeyote ambaye atafanya ubaguzi ndani ya mtandao huu ni sawa na kufanya hivyo ndani ya Old Trafford na viwanja vyovyote vile duniani.
Hapa bongo tuliona ni jinsi gani Waziri, Dkt. Khamis Kikwangala alichokifanya mara baada ya mashabiki wa soka nchini kumbagua mchezaji wa kikosi cha Senegal, Kepri Diatta katika mitandao ya kijamii. Waziri alikemea vitendo vile kwa nguvu sana na baadae kutumia uwanja huo wa mitandao ya kijamii kuhimiza upendo, kuheshimiana bila kujali itikadi, rangi au dini. Pia, kiongozi huyo aliwakumbusha kuwa waasisi wa taifa letu, walijenga taifa letu katika misingi ya kuheshimiana bila kujali dini, rangi au kabila na baadae alitoa fursa kwa mchezaji huyo kuja kutembelea mbuga zetu nchini bure kabisa yaan kwa mualiko wa Wizara Mali Asili na Utalii.
Soka ni mchezo ambao umeunganisha mataifa, umeziba ukabila, umeponya makovu ya ubaguzi pamoja na kufanikisha umoja. Yeyote yule anayetumia ubaguzi kama mbinu ya ushindi, kusawasilisha hisia zake au njia ya kuudhi mtu au kikundi cha watu huyo siyo mwanamichezo wala hafai ata kuvishwa lebo ya wanamichezo. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema katika hotuba zake “Hakuna dhambi kubwa kama dhambi ya ubaguzi” kama mdau wa michezo napinga vikali sana ubaguzi iliofanywa kwa wachezaji Marcus Rashford na Paul Pogba.



Imeandikwa na David Andy
 
Mnawasema sana mashabiki Wa man U muwaache na mahaba yao....
Nimesoma heading tu lakini....
Hivi man u mlinipa nini jamani najaribu kuhamishia ushabiki kwenye umachinga nakwama kabisa haya mahaba.....alisikika shabiki mmoja Wa man u huko mwanakwerekwe..
 
Mnawasema sana mashabiki Wa man U muwaache na mahaba yao....
Nimesoma heading tu lakini....
Hivi man u mlinipa nini jamani najaribu kuhamishia ushabiki kwenye umachinga nakwama kabisa haya mahaba.....alisikika shabiki mmoja Wa man u huko mwanakwerekwe..
Hahahahaa
 
Back
Top Bottom