Ujinga ni adui wa ujenzi wa mataifa

Ujinga ni adui wa ujenzi wa mataifa

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kuna duniaya kazi na uwajibikaji. Kila binadamu ana wajibu fulani kwa jamii yake, familia yake, na kwa Taifa lake.


Mambo yote haya yanapelekwa mbele na kitu kimoja, Mapenzi ya kutaka kuona mabadiliko. Ya kutaka kuona maisha ya binadamu yana kuwa bora zaidi ya aliyonayo, na maisha ya jamii yakitengemaa na Taifa likipata nguvu.


Nguvu hii yaTaifa haiji hivi hivi. Inaletwa na watu waliojipanga. Inaletwa na watu wenye nia moja na dhamira moja. Kukua ni hatua. Lakini ukuaji wa kitu chochote kile unahitaji mazingira bora ili uwe endelevu.

Kwahiyo, Ni muhimu kwa jamii zetu kujipanga na kuwa zenye nia moja kama kweli zinahitaji mabadiliko. Jamii zetu ni lazima zijue ni wapi zinataka kuelekea. Matatizo yote tuliyonayo hayatoisha kama hatutajipanga na kama hatutakuwa wenye dhamira moja ya kuboresha hali za jamii zetu.

Ni ukweli usiopingika kama watu wetu mmoja mmoja na jamii zetu zikipata nguvu na Taifa letu litanyanyuka pia. Hali za kiuchumi za kila mmoja wetu zikinyanyuka na uchumi wa Taifa utanyanyuka pia.


Jukumu laujenzi wa Taifa hili si la mtu mmoja au wawili au kikundi cha watu fulani. Jukumu la ujenzi wa taifa hili ni la kila mmoja wetu. Mdogo kwa mkubwa na kuendelea kwa Taifa hili kuna mtegemea kila mmoja wetu. Kila mmoja wetu ni mshiriki katika ujenzi wa Taifa hili. Serikalini chombo kinacho ratibu mfumo tu, lakini ni lazima kila mmoja wetu atimize wajibuwake kwa kufanya kazi kwa bidii, ili Taifa hili liendelee.


Heshima yaTaifa hili iko mikononi mwa kila mmoja wetu ni lazima tufanye kazi kwaajili ya Taifa hili bila ubinafsi ili lisonge mbele. Ni lazima tujenge jamii za watu wawajibikaji na wachapakazi na matatizo mengi tuliyonayo yatapungua. Ni lazima tujenge uwajibikaji kwa familia zetu, jamii zetu na Taifa letu. Ni lazima tulee watoto wetu katika nidhamu na maadili. Ndipo tutakapopata maendeleo.


Hatutaweza kuendelea na aina ya mawazo tuliyonayo ya kuangalia kila kitu katika mtazamo waumimi. Ili tuendelee ni lazima tufute aina hizo za fikra na tuwe na fikra za utaifa zaidi, ili tujenge baadae bora kwa vizazi vyetu vijavyo. Aina za fikra tulizonazo hazitatufikisha mbali kama Taifa. Fikra hizi haziwezi kulilinda Taifa hili. Njia hii si salama na kamwe haina matumaini kwetu. Ni lazima tubadilike. Ni lazima tuwe wazalendo na wawajibikaji.


Tuna uwezo wa kujenga Taifa hili. Tuna nguvu hiyo ya kulinyanyua na kuwa Taifa kubwa duniani, kama tutakuwa tayari kulitumikia.
Tuna uwezo wa kunyanyua matumaini kwa mamilioni ya watu wa taifa hili waliokosa matumaini.


Nguvu hii iko ndani yetu kama tutakuwa tayari kujitolea kuleta mabadiliko. Kama tutakuwa wawajibikaji na wenye nidhamu.Bila nidhamu hatutaweza kulinyanyua Taifa hili. Wote sisi tunapenda kuliona Taifa hili likinyanyuka na kutuletea heshima na matumaini.

Tuna wajibu mbele yetu, wajibu wa kulinyanyua Taifa hili na wajibu huu ni wa kila mmoja wetu. Mfagia barabara na polisi, daktari na mwanajeshi, mhandisi na mkulima,mwanasheria na mwanasayansi, mwalimu na mhasibu. Wote tuna wajibu wa kujenga Taifa hili. Ni wakati sasa wa kunyanyua matumaini yetu, ni wakati sasa wa kurudisha akili zetu kujenga Taifa hili.


Mgawanyiko wetu hautoweza kutuwezesha kujenga Taifa hili. Umoja wetu utatufanikisha kujenga Taifa hili. Uwajibikaji wetu utatufanikisha kujenga Taifa hili. Kujitolea kwetu pasipo ubinafsi kutalinyanyua Taifa hili.


Kazi yetu kubwa sasa ni kunyanyua uzalendo kwa watu wetu wote. Sababu bila uzalendo hatutaweza kulijenga wala kulilinda Taifa hili. Ni lazima tulipende Taifa hili na kuliheshimu ili watu wa mataifa mengine watu heshimu. Ni wakati wakujitambua kwetu na kutafuta Nafasi yetu katika uso wa Dunia. Ni lazima tufanyekazi kunyanyua Taifa hili.

TumelikoseaTaifa letu. Tumelijaza ubinafsi, ufisadi, chuki na wizi. Ni lazima tuondoe ufisadi ili huduma zifike kwa watu wetu na Taifa letu liendelee.
Ni lazima tuondoe urasimu katika taasisi mbali mbali za serikali na kijamii. Wakati umefika sasa ni lazima tutambue kuwa kiongozi ni kuwajibika kwa watu, sio nafasi ya kujilimbikizia mali. Ili Taifa hili liendelee ni lazima tupate watu wenye malengo mema kwa Taifa na wenye dhamira ya dhati ya kubadili maisha ya watu na Taifa.


Tunaweza kulisongesha Taifa hili mbele kama kila mtu katika kila fani akitia juhudi,akitia maarifa ili kunyanyua Taifa hili na kuliletea sifa. Sisi sio Taifa la kuwa omba omba. Ni lazima tufanye bidii tujitegemee na tutumie tunachozalisha. Hii nguvu iko mikononi mwetu. Ni lazima tuwekeze katika elimu na tuzalishe watu walioelimika na wenye nidhamu. Nilazima tujenge jamii za watu walioelimika wazalendo na wenye nia njema kwaTaifa lao. Ni ukweli usiopingika kwamba umaskini dawa yake ni kufanya kazi, na ujinga kutafuta maarifa. Tunaweza kushika silaha hizo na kuangamiza ujinga naumaskini. Tunahitaji viongozi bora sio bora viongozi. Watakaoleta dira na matumaini kwa watu wote. Watakaoleta mwelekeo.


Nimekuwa nikiamini kila wakati Taifa hili linauwezo wa kuwa kubwa kuliko unavyofikiri. Kama tukijipanga na kujitolea. Tuna uwezo wa kulijenga Taifa hili kizazi baada ya kizazi.

Kama Baba wa Taifa alivyosema inawezekana kama kila mtu akitimiza wajibu wake. Ni lazima tulijenge Taifa hili ili iwe sehemu nzuri ya kuishi sisi, watoto wetu na vizazi vyengine vingi vijavyo.


Kwa miaka mingi busara, amekuwa mjenzi na mlinzi wa mataifa mengi. Na pale busara inapotoweka hatma ya vizazi huwa mashakani.
Ndugu zangu ubinafsi na ufisadi huleta mgawanyiko katika jamii na matokeo yake ni vita na kile kidogo tulichokipata kwa ufisadi kitapotea na jamii yetu na Taifa letu litaparaganyika.

Usalama wetu kama Taifa upo katika utawala wa sheria na haki. Ndipo amani itakapo tamalaki.


Sisi ni kaka na dada, shangazi na mjomba na kila mmoja wetu ana nafasi na haki sawa katikaTaifa hili. Ni lazima tulijenge Taifa hili katika misingi ya haki. Tusiibie taasisi zetu za fedha, tuna libomoa Taifa letu wenyewe na tunaweka hatarini baadae yetu kama Taifa.

Mwisho nasema ujinga ni adui wa ujenzi wa mataifa. Watu wajinga wataangamia na mataifa yao kamwe hayatanyanyuka. Ni lazima tubadilike na tutambue sisi ni wamoja na baadae yetu ni moja.


Kama wazazi tunawajibu wa kujenga Taifa bora kwa watoto wetu. Hili ni jukumu letu sote. Tunahitaji mbadiliko ya fikra na moyo. Ni lazima tupambane na ujinga na kujenga Taifa la watu wenye nidhamu kwakuwa bila nidhamu hatutaweza kujenga chochote cha maana.
 
Back
Top Bottom